Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kuongezwa muda wa kamati ya kufuatilia silaha za maangamizi

Ban akaribisha kuongezwa muda wa kamati ya kufuatilia silaha za maangamizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kwa furaha hatua ya kuongezewa muda kamati iliyopewa jukumu la kufuatilizia azimio la umoja huo linalotaka kupigwa marafuku uzalishaji wa silaha za maangamizi.

Akizungumzia hatua hiyo iliyofikiwa na baraza la usalama hapo jumatatu, Ban amesema kuwa maeneo ambayo yalisaulikwa wakati wa utendaji wa kamati hiyo sasa yatafikiwa na kufanyiwa kazi. Aidha wiki iliyopita azimio hilo lilipendekeza kwa Katibu mkuu kuunda jopo la wataalamu nane ambao watafanya kazi pamoja na kamati hiyo.