Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muda wa UNMIS Sudan umeongezwa hadi 9 Julai

Muda wa UNMIS Sudan umeongezwa hadi 9 Julai

Wajumbe wa varaza la usalama leo wameafiki kuongeza muda wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa wakati wa miwsho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya Kusini na Kaskazini mwa Sudan na kuanzisha mpango mpya baada ya Sudan Kusini kujitenga rasmi mwezi Julai.

Katika azimio la bila kupingwa wajumbe wote 15 wamepiga kura kuongeza mpango wa UNMIS hadi Julai 9, tarehe ambayo Sudan Kusini itakuwa taifa huru na kujitenga na Sudan Kaskazini. Mamilioni ya raia wa Sudan Kusini walipiga kura ya maoni mwezi Januari ili kujitenga na Kaskazini kufuatia makubaliano ya amani ya CPA ya mwaka 2005 yaliyomaliza vita vya miongo kadhaa.

Katika azimio la leo baraza limesema lina mpango wa kuanzisha mpango utakaochukua nafasi ya UNMIS na limemuomba Katibu Mkuu Ban Ki-moon kuwasilisha ripoti ifikapo Mai 16 ya mipango ya Umoja wa Mataifa baada ya uhuru wa Sudan Kusini.