Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka uchunguzi dhidi ya mauaji Syria

Ban ataka uchunguzi dhidi ya mauaji Syria

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametaka kufanyika kwa uchunguzi kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Syria baada ya vikosi vya serikali kuongeza matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji nchini humo.

Katibu Mkuu huyo, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vifo na vikosi vya usalama kutumia vifaru na risasi za moto na amevitaka vikosi hivyo vya serikali kusitisha mara moja hujuma zake.

Amesisitiza haja ya kuwepo mageuzi ya kweli ili kukithi haja ya wananchi na kuongeza kuwa kutokana na hali ya mambo ilivyojiri kuna umuhimu mkubwa kwa kufanyika uchunguzi. Baraza la usalama limeanza kukutana kujadilia hali inavyoendelea sasa nchini Syria lakini hata hivyo hakuna ishara ya kufikia makubalino ya pamoja.