Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inasaidia kuimarisha soko la mbegu Afrika

FAO inasaidia kuimarisha soko la mbegu Afrika

Mtandao wa Afrika wa kupima na kuzijaribu mbegu katika maabara FAST, umeanzishwa ili kuimarisha soko la mbegu za mazao mbalimbali barani humo.

Mtandao huo umeanzishwa na muungano wa Afrika na mtandao wa mbegu kwa msaada mkubwa wa shirika la chakula na kilimo FAO.

Mtandao wa FAST ambao mwanzo makao yake yatakuwa Nairobi Kenya utaharakisha utekelezaji wa sheria za kuboresha sekta ya mbegu, kuzifanyia majaribio na kudhibiti ubora wa mbegu ikiwa ni pamoja na kuwa na taratibu za kuzipima mbegu za mazao makubwa kwa upande wa makampuni ya sekta za umma na binafsi. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)