Mahojiano

Pasipo na amani, Tanzania tunakwenda kuleta amani- Balozi Mahiga.

Tanzania imesema licha ya kupoteza askari wake kwenye operesheni za ulinzi wa amani, bado itaendelea kushiriki kwenye operesheni  hizo kwani inatambua kuwa bila amani hakuna maendeleo.

Sauti -
4'39"

Haipaswi kua ni chaguo baina ya kifo na uhai katika huduma ya afya: WHO

Huduma ya afya inapaswa kuwa ni haki ya binadamu na haipaswi kumpa mtu chaguo la kifo au uhai, kwa sababu tu anashindwa kumudu gharama za matibabu. 

Sauti -
2'14"

Vizuizi visivyo rasmi vyadororesha biashara Afrika Mashariki

Nchi za Afrika zinatarajiwa kutia saini makubaliano ya kuwa na eneo huru la biashara barani humo. Hii inakuja baada ya majadiliano ya muda mrefu wakati huu ambapo tayari maeneo ya ushirika wa kiuchumi.

Sauti -
7'23"

Elimu ndio mkombozi wa msichana wa kimasai

Ukosefu wa usawa kati ya maeneo ya mijini na vijijini ni kikwazo kwa maendeleo ya jamii. Na tofauti hiyo inazidi zaidi pindi jamii hiyo ina wanawake ambao kwao mahitaji yao yanapuuzwa licha ya kwamba wana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii zao.

Sauti -
2'8"

Nchi za Afrika zenye vita zaweza kujifunza toka Liberia

Penye nia pana njia, na kauli hiyo iliwafanya Waliberia kushikamana na kusema sasa vita basi. Wakafanya uchaguzi wa kidemokrasia na hadi sasa wanalia kivulini matunda ya amani waliyochumia juani. Nchi za Afrikazilizo vitani zifuate nyayo.

Sauti -
3'5"

Mahojiano na mbunge wa Kenya kuhusu uhamiaji

Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwa  makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.

Sauti -
3'53"

Radio haifi ng'o

Ujumbe wa siku ya radio duniani mwaka huu wa 2018 ni Radio na Michezo! Umoja wa Mataifa unataka chombo hicho adhimu kitumike kusaidia watu kuchanua na kuonyesha uwezo wao wote.

Sauti -
5'10"

Wanaume hawana hofu tena kuoa wasichana wasiokeketwa- UNFPA

Ali Haji Hamad, Afisa Jinsia wa UNFPA Tanzania anaangazia; 

Hali ya ukeketaji nchini Tanzania hivi sasa iko vipi?

Sauti -
6'15"

Penye nia pana njia- Mikoko Pamoja

Wakazi wa Gazi na Makongeni huko Kwale mjini Mombasa nchini Kenya waliamua kushikamana na kulivalia njuga suala la uhifadhi wa mazingira kwa kuanzisha mradi ambao pia unawakwamua katika umasikini.

Sauti -
4'11"