Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wahamiaji Afrika wasaka hifadhi Afrika

Wahamiaji kutoka Afrika kwenda Afrika! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kuhusu  maelfu ya wasaka hifadhi na wakimbizi walioko nchini Misri ambao wanasaidiwa na shrike la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi  UNHCR.

Kamishna Mkuu wa UNHCR amewatembelea wasaka hifadhi hao na kuzungumza nao  ili kuwasaidia.

Ungana na Amina Hassan katika makala ifuatayo.

UN Photo/Martine Perret

Umoja wa Mataifa na usaidizi nchini Burundi kwa mwaka huu wa 2016

Katika mfululizo wa makala za kuangazia kazi za Umoja wa Mataifa katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, tumejikita Burundi nchi ambayo mwaka jana ilikumbwa na sintofahamu ya kisiasa kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Usalama, na wawakilishi wake walifanya kazi ngumu ya kusaka suluhu ya kisiasa baada ya Rais wa nchi hiyo Piere Nkurunzinza kugombea mhula wa tatu wa Urais licha ya utata wa katiba, hatua iliyozua tafrani katika taifa hilo la kwani upinzani ulisusuia uchaguzi ukipinga hatua hiyo na hivyo kuzua machafuko.

Maisha ughaibuni: Mhamiaji asimulia visa na mikasa, sehemu ya 1

Hivi karibuni dunia imeadhimisha siku ya kimatiafa ya wahamiaji, siku ambayo haungazia ustawi, fursa na changamoto ya kundi hilo. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la wahimiaji duniani IOM, kwa zaidi ya wahamiaji milioni 240.

IOM inasema kuwa kundi hilo linakabiliwa na madhila kama vile ubaguzi, katika safari na hata nchi wanazofikia wakati wa kuhama. Ungana na Joseph Msami katika sehemu ya kwanza ya mahojino ya kusisimua na mhamiaji Mirara Jogu kutoka Kenya anayeelezea fursa na madhila kadhaa ikiwamo kutiwa nguvuni na polisi.

Mkate na maji ndio tegemeo Haiti

Tangu kimbunga Matthew kipige Haiti tarehe Nne Oktoba mwaka huu, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema bado mamia ya maelfu ya mamia ya watoto nchini humo hawana makazi wala chakula, hawaendi shule na wamo hatarini. Kimbunga hicho kilichoporomosha majengo, na kusomba mimea na miondombinu kimeacha nchi hiyo masikini katika hali mbaya zaidi. Mmoja wa waathirika ni mtoto mwenye umri wa miaka 15 na katika makala hii anatusimulia kile anachokipitia. Basi ungana na Flora Nducha kufahamu zaidi...

Watoa misaada waenziwa

Kila siku watoa misaada ya kibinadamu, wanawake kwa wanaume, popote ambapo msaada unahitajika, wao hujitolea ili kupunguza mateso na kuleta matumaini kwa wale wanaouhitaji zaidi.

Mara nyingi kazi hiyo huwapeleka katika maeneo hatarishi na wengi wao hupoteza maisha yao wakati wakifanya kazi hiyo. Ungana na Amina Hassan katika makala ifuatayo ya kumbukizi ya kazi ya watoa misaada ulimwenguni.

Grandi akutana na wakimbizi Niger

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi akiwa ziarani Niger, alitembelea mkoa wa Diffa, eneo moja ambalo watu zaidi ya 250,000 walipoteza makazi yao kufuatia mashambulizi wa kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.  Ziara ya Niger ni sehemu ya safari ya siku kumi ikiwa ni pamoja na kutembelea nchi za Chad, Cameroon na Nigeria ili kuyamulika mahitaji ya watu zaidi ya milioni 2  Katika ziwa la Chad waliotawanywa na Boko Haram na kutoa wito kwa jumuiya ya Umoja wa Kimataifa kushughulikia masilahi yao.

Baada ya kunusurika kwa Boko Haram, Firdau alenga kusaidia watoto

Jimbo la Borno, Kaskazini mashariki mwa Nigeria ni eneo lililoathirika zaidi kufuatia machafuko ya kundi la Boko Haram yaliyoanza karibu miaka miwili iliyopita. Mgogoro huo umesababisha wananchi wengi kupoteza makazi, miongoni mwao ikiwa ni watoto na wasichana wengi wakitekwa nyara na wapiganaji wao.

Kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, watoto millioni 28 wamepoteza makazi kutokana na vita na vurugu kote ulimwenguni.

UN Photo/Amanda Voisard

Watu wenye ulemavu Tanzania wataka mtandao wa kupaza sauti zao

Umoja wa Mataifa unasema watu wenye ulemavu wanahitaji kupewa kipaumbele katika sera, mipango na huduma mbalimbali ili wajumuishwe katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 20130 ambayo nchi wanachama wa umoja wa huo zinapaswa kutimiza.

Nchini Tanzania kundi hilo linapigia chepuo juhudi za mtandao wa kuwasaidia watu wenye ulemavu . Ni hatua zipi wanazochukua? Ungana na Tumaini Anatory  wa redio washirika Karagwe Fm ya Kagera Tanzania.

Ukitaka ujuzi anza kujitolea: Aloo

Kujitolea hukuza ujuzi, lakini pia huleta utoshelevu, ni maneno ya mbobezi katika kujitolea ambaye ni Afisa Programu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea UNV nchini Tanzania Josep Aloo katika mahojiano na Afisa wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchni humo Stella Vuzo.

Bwana Aloo ambaye anaratibu maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kujitolea Disemba tano, kwa Tanzania, amesema jamii bado ina uelewa mdogo kuhusu kujitolea jambo linalohitaji kupigiwa upatu zaidi.

Hapa anaanza kwa kueleza kitakaochofanyika mwishoni mwa juma katika kuienzi siku hiyo adhimu.