Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi wa ndani Sudan Kusini washerehekea Krisimasi

Hebu fikiria, Kusherehekea krisimasi katikati ya machafuko! Hali hii iliwakumba wakimbizi wa Sudan Kusini taifa ambalo kwa takribani miaka mitatu sasa limeshuhudia mapigano na hivyo kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Ungana na Joseph Msami katika makala itakayokupeleka kambini ambako wakimbizi hao wa ndani walisherehekea Krisimasi.

Muarobaini wa kutokomeza kipindupindu ni usafi: Dk Azma

Mlipuko wa ugonjwa kipindupindu ulioanza Agosti 15 mwaka huu nchini Tanzania unaendelea kugharimu mamia ya maisha ya watu kwani ugonjwa huo sasa umesambaa katika mikoa 21 ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Hata hivyo wadau wa afya wakiratibiwa na shirika la afya ulimwenguni WHO na mamlaka za afya za serikali wanahaha kunusuru maisha zaidi kwa mikakati ya kutoa elimu kwa uma. Dk Azma Simba kutoka wizara ya afya, ambaye ni mtaalamu wa afya ya jamii katika fani ya epidemiolojia amemweleza Joseph Msami wa idhaa hii katika mahojiano maalum hali ya kipindupindu ilivyo.

Madhila na usaidizi kwa wakimbizi wa Sudan

Maisha ukimbizini hujawa na taabu na mateso mengi. Hofu hutawala, kukosa makazi huambatana na kadhia hizi.

Nchini Sudan machafuko bado yanaendelea na hivyo kulazimu maelfu ya raia kukimbilia nchi jirani Sudan Kusini ambayo nayo mambo si shwari.Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

UN Photo/JC McIlwaine

Tanzania haina polio tena, siri ni kuwasaka wagonjwa kila kona: Dk Mbando

Baada ya safari ya muda mrefu ya kukabiliana na ugonjwa wa Polio unaosababisha kupooza kwa viungo vya mwili, Tanzani hatimaye imetngazwa kuwa imefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo.

Tangazo hilo lililotolewa na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la afya ulimwenguni WHO, pamoja na la kuhudumia watoto UNICEF, linalezwa kuwa ni juhudi za pamoja za wizara ya afaya ya nchi hiyo na wadau wa afya.

Michezo huvunja mipaka ya ubaguzi:UM

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya michezo kwa maendeleo na amani, na kamisheni ya haki za binadamu OHCHR kwa kushirikiana na nchi kadhaa zimeandaa tukio michuano ya mpira wa miguu sambamba na siku ya kimataifa ya haki za binadamu inayoadhimishwa kila tarehe 10 Disemba.

Ni tukio lililovunja mipaka ya aina zote za ubaguzi wa kila aina ambapo watu wa rangi, historia na hata mataifa mbalimbali , walijumuika. Ungana na Joseph Msami aliyeandaa makala ifuatayo.

Ripoti ya maendeleo ya binadamu yapambanua kile kinachopaswa kufanyika:UNDP

Hii leo imezinduliwa ripoti mpya kuhusu maendeleo ya binadamu ikitanabaisha yale yanayopaswa kuzingatia ili fursa zitokanazo na maendeleo ya teknolojia ziweze kuwa na manufaa kwa wote pindi linapokuja suala la ajira na maendeleo endelevu. Mathalani ripoti hiyo iliyoandaliwa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, inasema kuwa maendeleo ya teknolojia yamerahisisha utendaji kazi lakini wanufaika ni wachache, wanawake nao wakiwa wahanga zaidi kwani kile wanachofanya kinakuwa nje ya mfumo rasmi wa ajira kinakuwa hakihesabiwi na hata hakitambuliwi.

Mbivu na mbichi Jumamosi:COP21

Mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ulioanza juma lililopita ulipaswa kukamilika Ijumaa! Lakini vuta ni kuvute ya mashauriano imesogeza mbele mkutano kwa siku moja zaidi.

Nini majaliwa ya dunia ambayo imeelekeza macho na masikio Paris? Tuungane na Amina Hassan.

Muziki watumika kama chombo cha matumaini kwa wakimbizi kutoka Mali

Ghasia zikiiibuka katika nchi, watu hulazimika kukimbia na kuwaacha jamaa zao na mali zao. Nchini Mali wakati mapigano yalipoanza mwaka 2012 watu walikimbilia nchi jirani ikiwemo Mauritania.

Wakiwa ukimbizini,  akimbizi hawa wanajinasibu kwa nyimbo kama chombo cha kuunganisha jamii na kutoa matumaini na hata kuendeleza utamaduni wao. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.

Vijana wavuvi na makabiliano dhidi ya Ukimwi Uganda

Siku ya Ukimwi duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe mosi Disemba pamoja na mambo mengine hutumiwa na wadau kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa huu.

Hatua za uelimishaji wa makundi mbalimbali umefanyika nchini Uganda ambapo mwandishi wetu John Kibego anamulika mitazamo ya vijana wa Ziwa Albert magharibi mwa Uganda, kuhusu mambukizi ya virusi vya Ukimwi, hasa baada ya juhudi za uhamasishaji.

(Makala ya John Kibego)