Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wapatiwe nafasi katika sayansi na teknolojia, watasongesha agenda 2030- Mwanaisha Ulenge

Wanawake wapatiwe nafasi katika sayansi na teknolojia, watasongesha agenda 2030- Mwanaisha Ulenge

Pakua

Ikiwa imesalia takribani miaka 6 ushehe kufika mwaka 2030 muda ambao ulimwengu ulijiwekea lengo la kuwa umetimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), mapema mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiamini wanawake wanasayansi wana uwezo wa kuchangia haraka katika maendeleo ya ulimwengu, alieleza namna kuwanyima fursa za sayansi wanawake kunarudisha maendeleo nyuma na hivyo akashauri wanawake wanasayansi wapewe nafasi kuanzia darasani, maabara na katika vyumba vya maamuzi.

Mwanaisha Ulenge ni Mwanamke Mwanasayansi Mhandisi, Mbunge nchini Tanzania vilevile Mjumbe wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU) na hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa nilipata fursa ya kujadiliana naye kuhusu nafasi ya mwanamke katika sayansi na teknolojia.

Audio Credit
Anold Kayanda/Mwanaisha Ulenge
Sauti
7'17"
Photo Credit
UN/Anold Kayanda