Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wachukue hatua kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanatimizwa - Job Nyangenye Omanga

Vijana wachukue hatua kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanatimizwa - Job Nyangenye Omanga

Pakua

Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeingia siku yake ya nne hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wanakutana kujadili hatua za kuchukua ili  kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Mmoja wa wanaoshiriki ni Job Nyangenye Omanga, raia wa Kenya anayeishi Texas-Marekani akijishughulisha na sekta ya afya hapa Marekani na nyumbani Kenya. Mwenzangu Anold Kayanda amezungumza naye na kwanza Omanga anaanza kueleza ujumbe aliokuja nao kwenye Jukwaa hili.

Audio Credit
Leah Mushi/Anold Kayanda
Audio Duration
5'14"
Photo Credit
UN News