Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wanawake Burundi wajikwamua kiuchumi

Nchini Burundi mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga anatufahamisha kuwa licha ya wanawake wa nchi hiyo kupitia historia ya migogoro kutokana na baadhi yao kuwa wakimbizi ikiwa ni matokeo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, hilo halijawazuia kujishughulisha kikamlifu na shughuli mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Ungana na Kibuga katika makala inayofafanua zaidi juhudi za wanawake nchini Burundi.

Wadudu watumika katika harakati za ulinzi wa mazingira, ziwa victoria

Wakati tukielekea ukomo wa malengo ya milenia mwakani lengo namba saba ambalo ni utunzaji wa mazingira limefikiwa kwa kiasi na nchi mabli mbali. Moja ya sehemu ya muhimu ya uhifadhi katika mazingira ni uhifadhi wa maji. Katika makala hii Martin Nyoni wa radio washirika radio SAUT amevinajri katika mwambao wa ziwa Victoria na kutuandalia makala kuhusu naman wadudu wanatumika kuhifadhi ziwa hilo. Ungana naye.

Haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino

Tamko Umoja wa Mataifa  la haki za binadamu ni nguzo muhimu katika kulinda, na kutetea haki za makundi yote katika jamii kwa kuzingatia heshima na utu wa binadamu yeyote popote alipo.Tamko hilo la mwaka 1948 limetiliwa saini na nchi mbalimabli duniani wakiahidi kulinda haki za watu wao katika Nyanja mbalimbali. Miongoni mwa makundi yanayopaswa kulindwa ni watu wenye ulemavu ambao mara kadhaa hawatendewi haki kutokana na hali zao. Watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino ni sehemu ya kundi hilo.

Bodaboda, muziki vyatumika kusambaza elimu ya Ebola

Huko Afrika Magharibi, mbinu mbalimbali zinatumiwa katika kuhakikisha elimu ya mapambano dhidi ya Ebola inawafikia walengwa. Miongoni mwa mbinu hizo yakinifu ni kwa kupitia wanamuziki ambao wanafikisha ujumbe kirahisi kwa jamii kupitia tasnia ya burudani.

Mbali na mbinu hiyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa kushirikiana na serikali ya Sierra Leon wanatumia pikipiki maarufu kama bodaboda katika kufikisha elimu kwa umma. Ungana na Joseph Msami katika Makala inayofafanua vyema makabiliano haya dhidi ya homa kali ya Ebola.

Masahibu yanayowakumba wahamiaji

Tarehe 18 Disemba kila mwaka dunia ni siku ya wahamiaji duniani. Hii ni siku mahususi kwa ajili ya kuangazia ustawi wa kundi hili ambalo kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM,  ni zaidi ya watu milioni mia mbili kote duniani.

Maadhimisho ya siku hii yalipitishwa rasmi na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Disemba 4, mwaka 2000 kutokana na idadi kubwa ya wahamiaji inayoongezeka.

Hii ilitanguliwa na mkataba wa kimataifa kuhusu ulinzi wa haki za binadamu kwa wafanyakazi wote, wahamiaji na familia zao.

UNICEF, Oliver Mtukudzi wapambana na unyanyapaa dhidi ya waathirika wa HIV Tanzania

Unyanyapaa dhidi ya waaathirika wa ugonjwa wa ukimwi unatajwa kuwa tatizo kubwa katika jamii hususani barani Afrika. Katika kukabiliana nalo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF kwa kushirikiana na mwanamuziki mashuhuri barani humo Oliver Mtukudzi linafanay kampeni maalum ya kukomesha unyanyapaa kwa waathirika wa HIV.

Ungana na Joseph Msami katika Makala inayoangazaia kampeni hiyo nchini Tanzania

Utumwa mamboleo bado ni kikwazo

Wiki hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumezinduliwa muongo wa watu wenye asili ya bara la Afrika. Muongo huo unaoanza mwaka 2015 hadi 2024 unalenga kutoa fursa ya mtazamo mpya wa jamii hiyo ambayo imeenea maeneo mbali mbali duniani kuanzia barani Ulaya, Amerika hadi Asia. Je nini kilifanyika wakati wa uzinduzi huo? Ungana na shuhuda wetu Abdullah Boru.

Harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania

Kuanzia Disemba mosi hadi disemba 12 kumefanyika mkutano wa 20 wa nchi wanachama kuhusu masuala ya mazingira, COP20 huko Lima, Peru. Mkutano huo ulikuwa sehemu ya majadiliano ya kuwezesha kufikiwa na mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi mwakani huko Paris, Ufaransa.Majadiliano haya yanafanyika wakati tayari nchi zimeshuhudia athari za mabadiliko za tabia nchi ikiwemo:mmomonyoko wa udongo, ongezeko la kiwango cha maji ya bahari na athari zinginezo ambazo zimeathiri maisha ya watu. Basi ungana na Joseph Msami katika ripoti ifuatayo.

Picha:UNICEFTZ Facebook

Tanzania na harakati za kujikwamua kutoa elimu kwa wote

Elimu ya msingi kwa wote ni lengo namba mbili la maendeleo ya milenia (MDGS) linalosisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na elimu kwa wote ili kuwezesha maendeleo katika sekta zote. Nchini Tanzania licha ya changamoto kadhaa nchi hiyo inajitutumua kuhakikisha lengo hilo linatimizwa siyo tu kwa ujenzi wa madarasa lakini pia kuongeza kiwango cha uandikishaji shuleni.

Ungana na Jackson Sekiete wa radio washirika Morning Star katika makala ifuatayo.