Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wanaweza kutumia elimu yao kusongesha SDGs iwapo watapata ufadhili wa miradi yao - Gibson

Vijana wanaweza kutumia elimu yao kusongesha SDGs iwapo watapata ufadhili wa miradi yao - Gibson

Pakua

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa  kuhusu malengo ya maendeleo endelevu  kwa kifupi HLPF linakaribia kufikia ukingoni na leo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana aliitisha kikao cha kando kuzungumza na vijana kuhusu tathmini yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa walioshiriki ni Gibson Kawago, mmoja wa viongozi vijana wa kusongesha SDGs. Nimezungumza naye kufahamu mambo kadhaa ikiwemo alichowasilisha kwenye mkutano huu.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'31"
Photo Credit
UN/ Anold Kayanda