Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

BAKITA

Mahojiano maalum kuelekea siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili - BAKITA

Kuelekea siku ya lugha ya Kiswa duniani itakayoadhimishwa Ijumaa wiki hii Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam amefunga safari hadi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini humo BAKITA lenye wajibu mkubwa wa kuendelea na kukuza lugha hiyo adhimu sio Tanzania na Afrika tu bali duniani kote  na kuketi chini na mhariri mwandamizi wa Baraza hilo Onni Sigalla. Wamejadili mengi lakini Onni anaanza kufafanua jukumu lake BAKITA.

Sauti
7'16"
UNIC Tanzania/Stella Vuzo

Nyanduga: Ibara ya 1 inabeba tamko la haki za binadamu kila nchi inawajibika kuitekeleza

Mwaka huu 2023 tamko la haki za binadamu lililopotishwa katika azimio la mwaka 1948 linatimiza miaka 75. Msingi wa azimio la tamko hilo ilikuwa ni vita ya pili ya Dunia ambayo iliifanya dunia kutafakari nje ya kuhakikisha haki, Amani na utulivu vinadumishwa duniani. Kwa kutambua mchango wa tamko hiloleo tunaangazia ibara ya kwanza.

Sauti
7'1"
UN News

Maji ni zawadi toka kwa mungu hivyo ni haki ya kila mtu: Fr. Benedict Ayodi

Mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa unaanza leo Machi 22 hapa makao makuu ukibeba maudhui hatua za ajenda ya kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wote, kwani hatua hizo za maji zinaongeza uhakika wa chakula, usawa miongoni mwa jinsia, zinahakikisha watoto wanasalia shuleni, zinafanya jamii kuishi kwa amani na kuchangia mazingira yenye afya.

Umoja wa Mataifa unamtaka kila mtu kuchukua hatua na sasa na shirika la kimataifa lisilo la kiserikalia la Wakapuchini wa Fraciscan ni miongoni mwa wanaochukua hatua hizo ili kuhakikisha rasilimali hii muhimu inamfikia kila mtu.

Sauti
7'17"
UN News/Devotha Songorwa

Mabadiliko ya sera kuhusu bahari ni muhimu

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu bahari unaendelea huko Lisbon, Ureno. Mkutano huu umeanza tarehe 27 mwezi huu wa Juni na utamalizika tarehe 1 Julai 2022. Kabla ya kuanza kwa kikao cha ngazi ya juu, mkutano ulitanguliwa na jukwaa la vijana likileta pamoja wanaharakati na wachechemuzi vijana kuhusu masuala ya baharí wakionesha ubunifu wao wa jinsi ya kutatua dharura ya baharí, kama alivyooiita Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres .Miongoni mwa washiriki ni kijana Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dare es salaam nchini Tanzania.

Sauti
1'32"
UN News Picha: Assumpta Massoi

Ujio wangu na ushiriki katika Jukwaa la watu wa asili umekuwa na matokeo chanya mashinani-Kiburo

Mkutano wa 21 wa Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, UNPFFII mwaka 2022 umefanyika kwenye makao makuu yake New York. Mkutano huo umewakutanisha watu wengi kutoka pembe zote za dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni Carson Kiburo kijana kutoka jamii ya watu wa asili ya Bondel la ufa kaunti ya Baringo nchini Kenya, amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii.

Sauti
9'13"
© UNICEF/Mulugeta Ayene

FAO yatoa ushauri kwa wafugaji pindi ukame unapotishia mifugo yao

Huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika ambako huko kwa kipindi kirefu sasa njaa na ukame vimekuwa tatizo kubwa. Mwezi uliopita wa Januari shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO lilitoa ombi la zaidi ya dola milioni 138 za ufadhili wa dharura ili kusaidia watu milioni 1.5 walio hatarini katika jamii za vijijini huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. Kufahamu hali halisi mashinani iko vipi, Leah Mushi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Dokta.

Sauti
6'44"