Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Siku ya kimataifa ya wahamiaji

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhamiaji Shirika la kimataifa uhamiaji IOM linasema kwamba ukosefu wa huduma za matibabu kwa wahamiaji ni jambo ya kutisha na ina inahitaji kushughulikiwa kwa dharura .  Jumbe Omari Jumbe wa shirika la IOM anafafanua amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa.

Siku ya kimataifa ya ulemavu

Ni bayana kwamba watu walemavu huwa wanapitia chamgomoto nyingi za kimaisha zikiwemo umaskini, ajira, ndoa na kusafiri kutoka eneo moja hali lingine.

Siku ya kimataifa ya walemavu inapoadhimishwa hapo kesho December 3, Jason Nyakundi wa Radio ya Umoja wa Mataifa amepata kuzungumza na Isaac Manyonge mhasibu ambaye amekuwa mlemavu tangu utotoni na kisha kutuandalia makala ifuatayo. Tega sikio….

(MAZUNGUMZO YA JASON NYAKUNDI NA ISAAC MANYONGE)

Kila mmoja anajukumu la kumlinda mwenzie na ukimwi

Katika siku ya ukimwi duniani wito umetolewa kwa kila mtu kubeba jukumu la kujilinda na kuwalinda wengine na maambukizi mapya ya ukimwi.

kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO na lile la kupambana na ukimwi UNAIDS kila mtu katika jamii zote duniani ana fursa ya kuchangia kuhakikisha kuna maambukizi mapya sufuri, unyanyapaa sufuri na vifo vitokanavyo na ukimwi sufuri.

Wanaanchi hawa wa Afrika wana maoni gani kuhusu siku hii? wasikilize

(MAONI KUHUSU SIKU YA UKIMWI)

Wananchi wa DR Congo milioni 32 wapiga kura leo

Wananchi milioni 32 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  wameshiriki hii leo katika uchaguzi mkuu ulioshuhudia wagombea 11 wakiwania wadhifa wa urais akiwemo rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila na mpinzani wake mkuu Etienne Tchisekedi.

Vilevile wagombea elfu 18 wamejitokeza kuwania nafasi 500 pekee za ubunge. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga amefuatilia siku ya kwanza ya upigaji kura na kutuandalia taarifa hii.

(RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)

Mamia ya wakimbizi wa Ivory Coast na Angola warejea nyumbani:IOM

Mamia ya wakimbizi ambao walihama makwao kutokana na mzozo wa uchaguzi ulioikumba Ivory Coast wameanza kurejea nyumbani kwa usaidizi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Pia shirika hilo  linaendelea kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Angola walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia kurundi nyumbani kwa hiyari yao.

Afisa wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua kuhusu jitihada hizo alipozungumza na Monica Morara wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)

Ugonjwa wa kisukari unaweza kuzuilika:UM

Shirikisho la kimataifa la maradhi ya Kisukari IDF na shirika la afya duniani WHO wanasema maradhi ya kisukari yanaweza kuzuuilika kwa watu kuzingatia masharti ikiwemo kula vyakula vinavyofaa, kufanya mazoezi, kupungza unene na kuepuka matumizi ya tmbaku.

Leo ikiadhimishwa siku ya kisukari duniani takwimu zinaonyesha kuwa watu takribani milioni 4 wanakfa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kisukari na wengi wao wanatoka nchi za kipato cha wastani na kipato cha chini.

Burundi yasema haitavunjika moyo licha ya wanajeshi wake kuuawa Somalia

Huko Burundi, Jeshi la nchi hiyo limesema kwamba halitavunjika moyo licha ya tukio la hivi karibuni nchini Somalia ambako walinda amani wake katika kikosi cha Amisom waliuwawa wiki iliopita. Hata hivo giza linaendelea kutanda kuhusu idadi ya wanajeshi waliouwawa.

Taarifa za kutofautiana zilitolewa, Al Shabab wakidai kuwauwa wanajeshi wa Burundi zaidi ya 70 huku Jeshi la Burundi likitangaza idadi ya wanajeshi wasiozidi kumi waliouwawa.

UM wathibitisha vikosi vya Kenya kuingia Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga leo amethibitisha kwamba vikosi vya jeshi la Kenya vimeingia Somalia.

Balozi Mahiga amesema amezungumza na maafisa wa Kenya na Somalia kuhusu hatua hiyo ambayo Kenya inasema imechukua kwa ajili ya usalama na  kukabili uhalifu unaoendeshwa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-shabaab.