Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN News/Devotha Songorwa

Mabadiliko ya sera kuhusu bahari ni muhimu

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu bahari unaendelea huko Lisbon, Ureno. Mkutano huu umeanza tarehe 27 mwezi huu wa Juni na utamalizika tarehe 1 Julai 2022. Kabla ya kuanza kwa kikao cha ngazi ya juu, mkutano ulitanguliwa na jukwaa la vijana likileta pamoja wanaharakati na wachechemuzi vijana kuhusu masuala ya baharí wakionesha ubunifu wao wa jinsi ya kutatua dharura ya baharí, kama alivyooiita Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres .Miongoni mwa washiriki ni kijana Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dare es salaam nchini Tanzania.

Sauti
1'32"
UN News Picha: Assumpta Massoi

Ujio wangu na ushiriki katika Jukwaa la watu wa asili umekuwa na matokeo chanya mashinani-Kiburo

Mkutano wa 21 wa Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, UNPFFII mwaka 2022 umefanyika kwenye makao makuu yake New York. Mkutano huo umewakutanisha watu wengi kutoka pembe zote za dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni Carson Kiburo kijana kutoka jamii ya watu wa asili ya Bondel la ufa kaunti ya Baringo nchini Kenya, amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii.

Sauti
9'13"
© UNICEF/Mulugeta Ayene

FAO yatoa ushauri kwa wafugaji pindi ukame unapotishia mifugo yao

Huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika ambako huko kwa kipindi kirefu sasa njaa na ukame vimekuwa tatizo kubwa. Mwezi uliopita wa Januari shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO lilitoa ombi la zaidi ya dola milioni 138 za ufadhili wa dharura ili kusaidia watu milioni 1.5 walio hatarini katika jamii za vijijini huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. Kufahamu hali halisi mashinani iko vipi, Leah Mushi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Dokta.

Sauti
6'44"