Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Dkt Salim azungumzia uongozi Afrika na mustakhbali wa Sudan Kusini

Mwaka 2013 umefikia ukomo. Barani Afrika, mengi yametokea na mengine yanaendelea kutokea. Mathalani kifo cha Mzee Madiba na mzozo unaoendelea Sudan Kusini na kufanya wanadiplomasia kuendelea kukuna vichwa vyao kila uchao kupata suluhu ya kudumu za mzozo huo ndani ya taifa hilo changa lililopaswa kuwa mfano. Je nini mustakhbali wa Afrika baada ya Mandela? Na vipi Sudan Kusini?.

Miaka miwili na nusu toka Sudan Kusini ipate uhuru, hali si shwari

Mwezi Disemba mwaka 2013 ni miaka miwili na Nusu tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake kutoka Sudan, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Badala ya kuwa ni kipindi cha shamrashamra na kutathmni mwelekeo wa Taifahilochanga zaidi duniani, ulimwengu ulishtushwa na taarifa za kuibuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Hali si shwari huko Bor, Malakal,Juba, Unity na kwingineko nchini Sudan Kusini wananchi wanahaha! Jumuiya ya kimataifa halikadhalika. Je nini kinaendelea? Jitihada gani zimechukuliwa kumaliza mzozo huo? Basi ungana na Assumpta Massoi katika makala hii..

Mapigano, mafuriko vyatatiza maisha ya raia Somalia

Wakati macho na masikio ya jumuiya ya kimataifa yakielekezwa nchini Sudan Kusini ambako kuna mapigano ya kikabila, nchi nyingine iliyoko pembe yaAfrika,Somalianayo inakabiliana na changamoto ya mapigano ya kikabila.

Mapigano hayo yamesababisha hali mbaya kwa raia ambao wameshindwa kufikiwa na  misaada ya kibinadamu kutokana na mafuriko kukumba eneo ambako makabila hayo yanapigana liitwalo Johwar. Ungana na Joseph Msami katika taarifa ifuatayo.

Miaka 50 ya uhuru wa Kenya yaenziwa New York

Taifa la Kenya limetimiza miaka 5o tangu lijipatie uhuru wake kutoka kwa wakoloni ,Uingereza. Sherehe za kitaifa zimefanyika nchini humo ambapo wananchi wa taifa hilo lililoko Mashariki mwa Afrika waliadhimisha sherehe hizo kwa mambo kadhaa ikiwamo mkesha maalum ulioshuhudia kupandisha tena bendera ya Kenya kitendo kilichofanyika baada ya kuishusha ya mkoloni.

Maafisa wa jeshi Sudani Kusini wafunzwa kuhusu ulinzi wa raia

Mafunzo maalum ya ulizni wa raia yaliyohusisha jeshila Sudani Kusini yamefanyika nchini humo huku kukiwa na taarifa za shambulio la kupinduliwa kwa serikali hatua iliyolaaniwa na Umoja wa Mataifa. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS umeendesha mafunzo hayo kwa kuzingatia umuhimu wa ulinzi wa raia katika maeneo yaliyokumbwa na migogoro. 

Makala ifuatayo inaelezea namna jeshi la nchi hiyo linavyonufaika na mafunzo hayo ambayo matokeo yake ni kuzidisha ulinzi wa raia ambao hutegemea jeshi la nchi hiyo. Ungana na Joseph Msami.

Ukatili wa kijinsia wamulikwa nchini Tanzania

Hatimaye siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza tarehe 25 mwezi uliopita, zimehitimishwa wiki hii ya tarehe 11 Disemba. Katika kipindi hicho harakati mbali mbali zilitekelezwa kupazia sauti mbinu za kutokomeza ukatili wa kijinsia, majumbani, sehemu za kazi, shuleni na kwingineko ili dunia pawe sehemu bora ya ustawi kwa kila mtu bila kujali  jinsi yake. Je nchini Tanzania hali iko vipi? Tuungane na Anthony Joseph wa Radio washirika WAPO FM kutokaDar es salaam,Tanzania.

 (PCKG MAKALA YA ANTHONY JOSEPH)

Raia wa Guatemala anayejitolea Tanzania aeleza jinsi anavyoithamini kazi hiyo

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kujitolea inaelezwa kuwa umuhimu wa siku hii ni katika kukuza amani na maendeleo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema  mchango wa wanaojitolea unatambulika.

Miongoni mwa wanaojitolea ni Nataly Monila raia wa Guatemala anayefanya kazi za kufundisha mkoani Tanga nchini Tanzania na katika mahojiano na Muhamed Hamie wa radio washirika Pangani Fm, Bi Monila anasema licha ya kwamba hapati ujira kwa kazi anayofanya lakini anaifurahia kwani inatimiza ndoto zake.

(Sauti Mahojiano-Monila)

Tofauti ya lugha yaleta mkwamo kwa wakimbizi wa DRC huko Uganda

Upatikananji wa elimu ni changamoto ambayo bado inakabili baadhi ya nchi barani Afrika kutokana na umaskini na mizozo ya kisiasa na kijamii. Wakati wa mizozo jamii hukimbia katika nchi jirani kutafuta hifadhi kuna baadhi ya changamoto na mojawapo ni lugha hasa kwa wanafunzi basi ungana na John Kibego wa radio washirika Spice FM nchini Uganda katika makala ifuatayo

(makala ya John Kibego wa Spice FM)