Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Uganda yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu-WHO

Kila mwaka nchini Uganda hutokea wastan wa visa1,850 vya kipindupindu na takriban vifo 45. Hii ni kwa mujibu wa waziri wa Afya wa Uganda Dkt Jane Ruth Acieng alipozungumza wakati wauzinduzi wa kampeni hiyo.

Visa vingi hutokea sehemu za Mashariki, kaskazini na kaskzini maghari mwa Uganda. Zoezi hili linadhaminiwa na  shirika la kimataifa la muungano wa chanjo ,GAVI na dawa inayotumika ya matone ndio inatumika kwa mara ya kwanza nchini Uganda.

Siraj Kalyango wa Idhaa hii amezungumza na waziri wa afya anehusika na shughuli za jumla , Dkt Sarah Opendi, kuhusu chanjo hii.

Sauti
2'41"
UN News/Assumpta Massoi

Japo inajitahidi, Tanzania bado ina kibarua cha kutimiza SDG’s: Assad

Tanzania imepiga hatua katika utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGS, lakini inakabiliwa na changamoto lukuki ambazo zisiposhughulikiwa malengo hayo hayatotimia ipasavyo. Hayo yamesemwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini humo (CAG) Profesa Musa Juma Assad, katika mahojiano maalumu na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini New york Marekani. Profesa Assad alikuwa akihudhuria mkutano wa kimataifa wa tathimini ya utekelezaji wa SDG’s na mchango wa ofis iza ukaguzi wa hesabu za serikali katika kufanikisha malengo hayo.

Sauti
10'25"

Pasipo na amani, Tanzania tunakwenda kuleta amani- Balozi Mahiga.

Tanzania imesema licha ya kupoteza askari wake kwenye operesheni za ulinzi wa amani, bado itaendelea kushiriki kwenye operesheni  hizo kwani inatambua kuwa bila amani hakuna maendeleo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa huko Dar es Salaam, Tanzania huku akitanabaisha kuwa pasipo na amani ndio Tanzania inakwenda kuleta amani.

Sauti
4'39"
Picha/ UN/Albert Gonzales Farran

Haipaswi kua ni chaguo baina ya kifo na uhai katika huduma ya afya: WHO

Huduma ya afya inapaswa kuwa ni haki ya binadamu na haipaswi kumpa mtu chaguo la kifo au uhai, kwa sababu tu anashindwa kumudu gharama za matibabu. 

Hayo yamesemwa na shirika la afya ulimwenguni WHO katikakuelekea siku ya afya duniani hapo Aprili 7. Flora Nducha amezungumza na Dr Hillary Kipruto wa WHO kuhusu kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni huduma ya afya kwa wote.

Sauti
2'14"
FAO/Olivier Asselin

Vizuizi visivyo rasmi vyadororesha biashara Afrika Mashariki

Nchi za Afrika zinatarajiwa kutia saini makubaliano ya kuwa na eneo huru la biashara barani humo. Hii inakuja baada ya majadiliano ya muda mrefu wakati huu ambapo tayari maeneo ya ushirika wa kiuchumi. Baadhi ya watu wana hofu kuwa pengine makubaliano hayo hayatakuwa na mashiko huku wengine wakiwa na matumaini makubwa ya mpango huo kuwa utapanua siyo tu wigo wa soko bali pia kufungua fursa za biashara.

Sauti
7'23"
UN News/Assumpta Massoi

Elimu ndio mkombozi wa msichana wa kimasai

Ukosefu wa usawa kati ya maeneo ya mijini na vijijini ni kikwazo kwa maendeleo ya jamii. Na tofauti hiyo inazidi zaidi pindi jamii hiyo ina wanawake ambao kwao mahitaji yao yanapuuzwa licha ya kwamba wana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii zao. Kutoka Arusha Tanzania, Assumpta Massoi amezungumza na Maria Mamasita mshiriki wa mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW62 ulioanza tarehe 12 mwezi huu wa Machi, mada kuu ikiangazia kumwendeleza mwanamke wa kijijini. Je wao wanafanya nini?

Sauti
2'8"