Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunawezesha wakulima wanawake Tanzania ili wapate masoko ndani na nje ya nchi - Matika Maiseli, TPHPA

Tunawezesha wakulima wanawake Tanzania ili wapate masoko ndani na nje ya nchi - Matika Maiseli, TPHPA

Pakua

Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya  hali  ya wanawake duniani, CSW68 umekunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataia jijini New York, Marekani na miongoni mwa washiriki ni Matika Maiseli, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Afya na Mimea na Viuatilifu, TPHPA iliyo chini ya Wizara ya Kilimo nchini Tanzania.

Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye kufahamu ni nini anaondoka nacho kutoka mkutano huu uliolenga kusongesha  usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake na kutokomeza umaskini.

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Sauti
3'9"
Photo Credit
UN News