Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii ni ushirikiano wetu - Fr. Benedict Ayodi

Siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii ni ushirikiano wetu - Fr. Benedict Ayodi

Pakua

Hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla la kupatia tuzo washindi wa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tuzo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja au kundi kwa kuzingatia mchango wao kwenye kusongesha haki za binadamu. Miongoni mwa washindi wa watano ni Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani. Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ni sehemu ya ushirikiano huo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya  Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Father Benedict Ayodi kutoka shirika hili kufahamu pamoja na mambo mengina sababu ya Ushindi wao. Lakini kwanza anaanza kwa kuelezea jinsi walivyopokea tuzo hii. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Sauti
7'46"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi