Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEA6 ni mwongozo wa kushirikisha pande zote katika kulinda mazingira: Irene Mwoga

UNEA6 ni mwongozo wa kushirikisha pande zote katika kulinda mazingira: Irene Mwoga

Pakua

Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya.  Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.

Irene Mwoga mtaalamu wa takwimu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa bara la Afrika ni Mratibu wa Mkutano huo amezungumza na Stella Vuzo wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Naironi Kenya UNIS na kuhusu mkutano huo dhamira ya mkutano huu unaofanyika kila baada ya miaka miwili, katika mwezi wa Februari akianza kwa kueleza UNEA6 ni nini..

Audio Credit
Anold Kayanda/Stella Vuzo
Audio Duration
2'23"
Photo Credit
UNIS/Stella Vuzo