Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
COP26
Wanawake wanabeba mzigo mkubwa wa janga la tabianchi – COP26
Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, COP26 unaoendelea mjini Glasgow nchini Uskochi umeonesha kuwa kundi la wanawake linachukua asilimia 80 ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi na kwa hivyo kundi hilo linabeba zaidi mzigo mkubwa wa janga la tabianchi.
Guterres ataja mambo manne ya kuzingatia kuleta ujumuishi, amani na usawa duniani
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , leo limekutana katika mjadala wa wazi kwenye makao Makuu mjini New York Marekani kuangazia ukarabati wa amani ya kimataifa na usalama , hasa katika upande wa kubaguliwa, kutokuwepo na usawa na migogoro.
Wakulima wabangladesh wateswa na mafuriko
Nchini Bangladesh mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni mwiba kwa maisha ya kila siku ya watu wa taifa hilo la Asia. Kwa mujibu wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD zaidi ya nusu ya watu milioni 90 wa nchi hiyo wanaishi katika maeneo yaliyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi huku wakikabiliwa na hatari kubwa ya mafuriko na wakulima ndio wanaobeba gharama kubwa ya zahma hiyo.
Wakulima wanabeba gharama kubwa ya mabadiliko ya tabianchi Bangladesh:IFAD
Nchini Bangladesh mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni mwiba kwa maisha ya kila siku ya watu wa taifa hilo la Asia. Kwa mujibu wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD zaidi ya nusu ya watu milioni 90 wa nchi hiyo wanaishi katika maeneo yaliyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi huku wakikabiliwa na hatari kubwa ya mafuriko na wakulima ndio wanaobeba gharama kubwa ya zahma hiyo.
Sekta ya mitindo ya nguo yatangaza mkakati kulinda tabianchi
Sekta ya ubunifu wa mitindo ya mavazi imetangaza hatua yake ya kuelimisha wazalishaji na wavaaji wa nguo dunia ili waweze kuvaa mavazi yao tena na tena kama njia ya kupunguza uzalishaji na ununuzi wa nguo kupitiliza ambao unachangia katika madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Nchi masikni zataka nchi tajiri zitimize ahadi zao za kuwapatia fedha
Mafuriko makubwa, mioto ya nyika inayoangamiza misitu, na kupanda kwa kina cha bahari pamoja na maelfu ya maisha ya watu yanayokatizwa na majanga hayo na riziki wza watu zinazoendelea kuathiriwa, ni hali halisi ambayo mataifa mengi tayari yanakabiliana nayo.
Fedha ndio mtihani mkubwa kwa nchi kukabiliana na afya na mabadiliko ya tabianchi:WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO leo limesema nchi nyingi zimeanza kuweka kipaumbele cha afya katika juhudi zao za kuwalinda watu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini ni takriban robo tu ya wale waliofanyiwa utafiti hivi karibuni na Shirika hilo wameweza kutekeleza kikamilifu mipango au mikakati yao ya kitaifa ya afya na mabadiliko ya tabianchi.
08 Novemba 2021
Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ya kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, leo tutakuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia ziara ya Waambata Jeshi kutoka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC ambao wanaziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa walipozuru wilayani Beni kujionea utendaji kazi wa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaounda Brigedi ya kujibu mashambulizi FIB MONUSCO.
COP26: Watu wa asili wana nafasi kubwa ya pekee katika kuzuia mabadiliko ya tabianchi
Mamilioni ya watu wameingia kwenye mitaa ya miji kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na viunga vya mji wa Glasgow nchini Uskochi unakofanyika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi COP26 wakidai hatua kubwa zaidi ya tabianchi huku nchi zinazoshiriki katika mazungumzo ya COP26 zikiwa zimeahidi kuwekeza katika masuluhisho yasiyoharibu tabianchi kupitia kilimo.
Vijana washika hatamu COP26 wakitaka vitendo kulinda tabianchi
“Tunataka nini? Haki kwa tabianchi! Tunataka lini? Sasa!” Kauli hizo zimesikika zikipazwa na vijana eneo lote la kati la mji wa Glasgow huko Scotland hii leo Ijumaa wakati maelfu ya waandamanaji walipoingia mitaa ya mji katika siku ambayo mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 ulitenga kwa ajili ya vijana