Jipime ufahamu wako kuhusu COP26

Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 unafanyika Glasgow, Scotland. Je unafahamu kwa kiwango gani yanayojadili? Hapa kuna fursa ya kujaribu uelewa wako kupitia maswali yetu kwako kuhusu mabadiliko ya tabianchi. (Majibu yako chini kabisa ya ukurasa huu)
(a) David Attenborough, mtangazaji wa vipindi vya televisheni.
(b) Margaret Thatcher, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza
(c) Greta Thunberg, mwanaharakati wa tabianchi kutoka Sweden
(a) George Clooney, mcheza filamu na mwanaharakati.
(b) Noël Godin kutoka Ubelgiji almaarufu Georges le Gloupier
(c) Barack Obama, wakati huo Rais wa Marekani.
(a) Mochie
(b) Dreich
(c) Drookit
7. Ni kikundi kipi cha muziki wa K-Pop kimetajwa kuwa mabalozi wema wa mkutano wa COP26?
(a) BTS
(b) BLACKPINK
(c) XTC
(a) NDC
(b) SDG
(c) PRI
(a) Huenda
(b) Uta
(c) Lazima
(a) Hatua muhimu kwa hatua kwa tabianchi.
(b) Kueleka katika janga la tabianchi.
(c) Alama nyekundu kwa ubinadamu
1. (b) Margaret Thatcher Waziri Mkuu wa zamani wa Uingreza akitambulika kama the “Iron Lady” au mwanamke wa shoka! Alisoma kemia Chuo Kikuu na hivyo alielewa tishio la mabadiliko ya tabianchi wakati alipotoa taarifa hiyo kwenye hotuba ya mwaka 1988. Mwaka uliofuatia alitoa matamshi sawa na hayo wakati wa hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliposema kuwa changamoto za mazingira zinazoikumba dunia nzima zinastahili hatua sawa kutoka dunia nzima.
2.Wavuti wa Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa Eritrea, Iran, Iraq, Libya na Yemen hazijaridhia Mkataba wa Paris.
3.(c) Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama. Wakati mkutano ulikaribia kuisha na bila ya makubaliano kati ya Marekani na kundi la nchi zikiwemo (Brazil, Afrika Kusini, India na China), Bwana Obama alipata habari kuwa viongozi wa nchi hizo walikuwa kwenye mkutano. Mbele ya vyombo vya habari aliwasili kwenye mkutano uliokuwa umehudhuriwa na Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh, Rais wa Brazil Luis Inacio Lula da Silva na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na kujitambulisha kwa sauti “mko tayari?”
4.Zote ziko kwenye hatari ya kuzama kabisa kufuatia kuongezeka kwa maji ya kina cha maji ya bahari miongo inayokuja. Kulingana na shirika la NASA, Mumbai itakuwa chini ya maji ifikapo 2050, utafiti unaonyeha kuwa Miami ni moja ya miji ya pwani iliyo hatarini duniani na visiwa vya Maldives vinavyotegemea sana utalii wanapanga kuwa na mji unaoelea angalau wabaki wakiwa wanaelea.
5.(c) Utabiri unasema mvua kubwa kwa hivyo jina “drookit” ndio muafaka la kuulezea mji wa Glasgow wiki ijayo.
6.Yote ina suluhu za asili za mabadiliko ya tabianchi. Misitu iliyo chini ya maji ina uwezo wa kuondoa viwango vikubwa vya hewa ukaa kutoka hewani
Mipango ya upanzi wa miti inapunguza kuharibika kwa ardhi na kuongezeka kwa gesi ya hewa ukaa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa linasena kuwa mikoko ni suluhu kubwa kwa tatizo la mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa ina uwezo wa kuhifadhi mara nne zaidi ya gesi ya kaboni kuliko misitu mingine.
7. (b) BLACKPINK waliteuliwa kuwa mabalozi wema wa mkutano wa COP26 mwezi Februari. BTS ni marafiki wa UN baada ya kushughulika na wajibu muhimu wakati wa mkutano wa mwaka huu wa UN hata kwa kutengenezea video ya muziki kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. XTC hata hivyo sio kundi la K-Pop bali bendi ya pop ya miaka ya 1970.
8. (a) NDC, ni kifupi cha Nationally Determined Contribution au mipango ya nchi kuchangia ili kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na hivyo kulinda tabianchi. SDG ni kifupi cha Sustainable Development Goals, au malengo endelevu yenye ukomo mwaka 2030 na PRI inamaanisha Principles for Responsible Investment, mtandao unoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa wataalamu katika sekta ya fedha inahusika na kuinua uwekezaji wa kudumu
9. (b) ‘Uta’ kwa kiingereza ‘shall.’ Sote tunakumbuka vilio na shangwe baada makubaliano ya Mkataba wa Paris, lakini nusura iwe kinyume. Nyakati za mwisho kundi la mawakili kutoka Marekani waligundua kuwa neno ‘shall’ lilikuwa kwenye kipengele muhimu kilichohusu kupunguza gesi chafuzi badala ya neno ‘should’. Suluhu kutoka kwa Wafaransa walioandaa mkutano huo ni kuwa yalikuwa ni makosa ya herufi.
10. (c) Alama nyekundu kwa ubinadamu. Ripoti hiyo iliundwa na wanasayansi 234 kutoka nchi 66 ikisema kuwa shughuli za mwanadamu zimeongeza joto duniani kwa kasi kubwa kwa takriban miaka 2000 iliyopita.Wakati wa uzinduzi wa ripoti ya shirika la mazingira la umoja wa Mataifa UNEP kuhusu gesi chafuzi katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alionya kuwa “tuko njiani kuelekea janga la mabadiliko ya tabianchi”.