Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 Novemba 2021

08 Novemba 2021

Pakua

Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ya kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, leo tutakuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia ziara ya Waambata Jeshi kutoka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC ambao wanaziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa walipozuru wilayani Beni kujionea utendaji kazi wa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaounda Brigedi ya kujibu mashambulizi FIB MONUSCO.

Lakini pia utasikia taarifa ya habari kwa ufupi ikiangazia mabadiliko ya tabianchi na njaa ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limeonya kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa katika nchi 43, imeongezeka hadi kufikia milioni 45, hili ni ongezeko la watu milioni tatu mwaka huu, huku njaa kali ikiongezeka kote ulimwenguni.

Audio Credit
Assumpta Massoi