Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Mauritania wapambana na mabadiliko ya tabianchi

siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 26 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, ambao hivi sasa unaendelea Glascow, Scotland, Mshauri Maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudunia wakimbizi, UNHCR kuhusu Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Andrew Harper ametembelea Mauritania kujionea jinsi wakimbizi wanavyopambana na janga la tabianchi.

(Taarifa ya John Kibego)
“Hatujawahi kuona mwaka kama 2021. Huu ni mwaka wenye mioto mingi ya nyika.” Anasema Ahmedou El-Bokhary, Rais wa Kikosi cha zima moto kinachoundwa na wakimbizi.  

Sauti
2'5"

04 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, leo ni siku ya kimataifa ya kupinga uonevu shuleni na mitandaoni ambapo UNESCO imetaka watoto kulindwa zaidi, WFP imetoa msaada kwa wananchi wa Madagascar wanaoishi katika ukame na hivyo kulazimika kula mmea wa Dungusi kakati.

Pia utasikia kauli ya Rais wa COP26 huko Glasgow kuhusu nchi tajiri kutoa fedha za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
13'18"
Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto zinazoikabili dunia. Ukanda wa Saheli kusini mwa jangwa la Sahara.
© UNDP Mauritania/Freya Morales

Kama sisi tumeweza, wengine washindwe kwa nini? – Wakimbizi Mauritania 

Hivi karibuni, siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, #COP26 ambao hivi sasa unaendelea Glascow, Uskochi, Mshauri Maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudunia wakimbizi, UNHCR kuhusu Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Andrew Harper ametembelea Mauritania kujionea jinsi wakimbizi wanavyopambana na janga la tabianchi.

Sauti
2'5"