Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Basi la National Express lisilotoa hewa chafuzi likiwa nje ya Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP26 huko Glasgow, Scotland.
UN News/Laura Quinones

Wakati umefika kugeukia usafiri unaolinda mazingira: COP26

Kuwa na dunia ambayo vyombo vya usafiri kama magari, mabasi na malori ambayo yanatumia umeme n ani ya gharama nafuu, kuwa dunia ambayo vyombo wa usafiri wa bahari vinatumia nishati safi pekee na ndege ziweze kusafiri kwa kutumia hewa safi ya Hydrogen inaweza kuonekana kama ndoto ama sinema lakini kwenye mkutano wa COP26 unaoendelea huko Glasgow serikali nyingi na makampuni ya biashara wamesema wameanza kutimiza ndoto hizi na kuzifanya kuwa hali halisi.