Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

05 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu Tsunami, na kama ilivyo ada leo ni mada kwa kina ambapo tunaangazia vijana na mchango wao katika mabadiliko ya tabianchi wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa COP26 ukiendelea huko Glasgow Scotland. 

Flora Nducha amezungumza na mmoja wa vijana wanaharakati wa mazingira kutoka nchini Kenya na mshindi wa tuzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP ya champion of the Earth 2020 kutokana na kampuni yake ya Change Makers kubadili taka za platiki kuwa tofali.

Audio Duration
13'7"