Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

State House Tanzania

Sasa tutoke kwenye maneno na ahadi, twende kwenye kufanya kweli kuhusu mabadiliko ya tabianchi: Rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameelezea kile ambacho taifa lake na nchi nyingine zinazoendelea wanataka kuona kinatekelezwa baada ya mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 unaofanyika huko Glasgow Scotland.

Amesema hayo punde baada ya kuhutubia mjadala wa wazi wa mkutano huo unaofanyika wakati nchi tajiri zikisuasua kutekeleza ahadi zao akiongeza kuwa

Sauti
2'32"
UN/ John Kibego

Jamii ya Watyaba kandoni mwa Ziwa Albert nchini Uganda yatishiwa tena na mafuriko

Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 unaendelea katika huko Glosgow na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa amewaeleza viongozi wa ulimwengu kuwa ni muhimu kuchukua hatua sasa kwani wanadamu wanajichimbia kaburi, nchini Uganda jamii ya Watyaba, mojawapo ya jamii za walio wachache wanaoishi katika viunga vya Ziwa Albert, wanapaza sauti kwa serikali na shirIka  la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kuwasaidia kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
3'45"
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akihutubia mjadala wa viongozi kuhusu mshikamano kwenye mkutano wa COP26 huko Glasgow, Scotland
UN WebTV Video

Tunapimwa kwa vitendo vyetu na si kwa ahadi kubwa kubwa- Rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza katika mjadala wa wazi wa viongozi kwenye mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, CO26 huko Glasgow, Scotland na kusema mshikamano na juhudi zao kama viongozi katika kukabili mabadiliko ya tabianchi vitapimwa si kwa ahadi kubwa wanazotoa kwenye mkutano huo bali kwa jinsi wanatekeleza vipengele vyote vya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.
 

Mabadiliko ya tabianchi yameongeza hatari ya hali ya hewa kavu, ya joto ambao inachangia kuchochea moto wa nyika
Unsplash/Mikhail Serdyukov

COP26 ikifungua pazia WMO yasema miaka 7 iliyopita imevunja rekodi ya joto duniani

Miaka saba iliyopita inaelekea kuwa ya joto zaidi kuwahi kurekodiwa sanjari na kupanda kwa kina cha bahari ni katika viwango vya kuvunja rekodi, kulingana na ripoti ya muda ya shirika la hali ya hewa duniani (WMO) ya hali ya hewa duniani kwa mwaka 2021, iliyotolewa Jleo umapili, wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26, ukifunguliwa Glasgow, Uingereza.