Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Wahudumu wa afya nchini Iran wakiangalia vifaa vya matibabu huku nchi hiyo ikiendelea kupambana na virusi vya corona.
WHO/Iran

Fedha ndio mtihani mkubwa kwa nchi kukabiliana na afya na mabadiliko ya tabianchi:WHO

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO leo limesema nchi nyingi zimeanza kuweka kipaumbele cha afya katika juhudi zao za kuwalinda watu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini ni takriban robo tu ya wale waliofanyiwa utafiti hivi karibuni na Shirika hilo wameweza kutekeleza kikamilifu mipango au mikakati yao ya kitaifa ya afya na mabadiliko ya tabianchi.

08 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ya kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, leo tutakuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia ziara ya Waambata Jeshi kutoka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC ambao wanaziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa walipozuru wilayani Beni kujionea utendaji kazi wa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaounda Brigedi ya kujibu mashambulizi FIB MONUSCO.