Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA 76 using tag UNGA76

MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
21 Septemba 2021-27 Septemba 2021

Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, #UNGA76 umefunguliwa Jumanne ya tarehe 14 mwezi Septemba mwaka 2021 kwenye makao makuu jijini New  York, Marekani. Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu utaanza Jumanne ya tarehe 21 mwezi Septemba mwaka 2021 na kumalizika tarehe 27 mwezi Septemba 2021. Katika ukurasa huu utapata taarifa motomoto kuhusu mjadala huo mkuu wa ngazi ya juu na matukio mengine ikiwemo miaka ufadhili kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi, mifumo ya chakula, maadhimisho ya miaka 20 ya azimio la Durban linalopinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zingine zote, mabadiliko ya tabianchi na ulinzi na usalama, masuala ya nishati  na pia kuenziwa kwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld.Vikao vingine vya ngazi ya juu vitakavyofanyika wakati wa wiki za mwanzo za #UNGA76 ni pamoja na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu COVID-19.  UNGA76 inafanyika wakati  janga la COVID-19 likiendelea kwa hiyo vikao vitafanyika moja kwa moja ukumbini makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini pia kwa njia ya mtandao ambapo baajhi ya wakuu wa nchi na serikali hotuba zao zitakuwa kititolewa kwa njia ya mtandao.

Tufuatilie katika majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

YouTube: https://www.youtube.com/c/UNNewsKiswahili

Twitter: https://twitter.com/HabarizaUN

UN Photo/Violaine Martin (file)

Mahojiano na Katibu Mkuu wa UN

“Ni wakati wa kupiga kengele ya dharura”, amesema Katibu Mkuu wa UN katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa siku chache kabla ya kuanza kwa Mjadala wa Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akihojiwa na Assumpta Massoi wa UN News, António Guterres amegusia ushirikiano wa kimataifa, harakati za utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 duniani, mabadiliko ya tabianchi, usawa wa jinsia, viijana, amani na usalama barani Afrika na duniani kwa ujumla

Sauti
9'34"
UN Photo/Violaine Martin (file)

Ni wakati wa kupiga kengele ya dharura- Guterres

“Ni wakati wa kupiga kengele ya dharura”, amesema Katibu Mkuu wa UN katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa siku chache kabla ya kuanza kwa Mjadala wa Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akihojiwa na Assumpta Massoi wa UN News, António Guterres amegusia ushirikiano wa kimataifa, harakati za utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 duniani, mabadiliko ya tabianchi, usawa wa jinsia, viijana, amani na usalama barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Sauti
9'34"
Rais wa UNGA76 Abdullah Shahid akifunga mjadala mkuu wa UNGA76 jijini New York, Marekani 27 Septemba 2021
UN/Cia Pak

Rais wa UNGA76 afunga pazia la mjadala mkuu; asema ushirikiano wa kimataifa ungali hai

Hatimaye mjadala mkuu wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA76 umefunga pazia leo Jumatatu katika makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani huku Rais wa Baraza hilo Abdullah Shahid akisema mkutano huo umefanyika kwa mafaniko makubwa katikati ya janga la Corona au COVID-19 huku akitaja sababu za mafanikio hayo kuwa ni hatua bora za kupunguza maambukizi na viwango vya juu vya chanjo.