Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Samia wa Tanzania miongoni mwa watakaokutana na Rais wa UNGA76

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania (kulia) katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Rebecca Nyandeng Garang jijini New York, Marekani ambako wanashiriki mikutano ya ngazi ya juu ya UNGA76.
Ikulu Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania (kulia) katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Rebecca Nyandeng Garang jijini New York, Marekani ambako wanashiriki mikutano ya ngazi ya juu ya UNGA76.

Rais Samia wa Tanzania miongoni mwa watakaokutana na Rais wa UNGA76

Wanawake

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ni miongoni mwa wakuu wa nchi na serikali ambao hii leo wanakuwa na kikao na Rais wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdulla Shahid.Mkutano huo maalum unafanyika kando mwa mjadala mkuu wa UNGA76 kwenye makao makuu ya UN jijini New York, Marekani.

Bwana Shahid mbaye anatambulika zaidi kama bingwa wa masuala ya usawa wa kijinsia amenukuliwa na kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi yake akisema amewakaribisha viongozi wanawake kubadilisha uzoefu wao na mambo waliyojifunza katika kuimarisha usawa wa kijinsia katika ngazi zote hasa katika viwango vya juu ambako idadi ya wanawake ni ndogo. 

Rais Shahid anaamini kuwa, "viongozi wanawake waliofanikiwa sio tu wanawakilisha kile kinachowezekana katika mapambano ya usawa wa kijinsia lakini wanaweza kutoa njia bora za jinsi ya kufikia kwenye usawa."

Viongozi wanawake wanafanya jukumu muhimu ya kuleta usawa duniani kote
UN Women
Viongozi wanawake wanafanya jukumu muhimu ya kuleta usawa duniani kote

Kando mwa Rais Samia wa Tanzania wengine waliokaribishwa ni Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheik Hasina, Rais wa Jamhuri ya Estonia, Kersti Kaljulaid, Rais wa Jamhuri ya Moldova, Maia Sandu, Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg, na Rais wa Tume ya Ulaya, Bwana Ursula von der Leyen.

"Wakati najivunia kubeba jina la 'bingwa wa kijinsia', nina unyenyekevu kutambua kwamba ninahitaji kusikiliza. Wanawake na wasichana wanahitaji kupaza sauti zao, uzoefu wao wa moja kwa moja, kusikilizwa na kutambuliwa. Ni nani bora kuzungumza juu ya wanawake katika uongozi kuliko wale wanawake ambao wamepanda hadi ofisi za juu zaidi?, "amesema Rais Shahid.

Mkutano huo unafanyika kando mwa vikao mbalimbali vinavyoendelea ikiwa ni siku ya kwanza ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambao unafanyika tarehe 21- 27 Septemba 2021. 

Rais Shahid anatarajiwa kujenga upya kikundi cha ushauri wa kijinsia kilichoanzishwa katika Baraza Kuu la mwaka 2020 ili kuhakikisha kuwa shughuli zote na utekelezaji wote wa vikao vya Baraza kuu mwaka UNGA76 unaonesha mtazamo wa kijinsia.