Ni wakati wa kupiga kengele ya dharura- Guterres

Huwezi kupewa madaraka bali unayatwaa, kwa hiyo tunahitaji wanawake kupigania haki zao kikamilifu
António Guterres , Katibu Mkuu wa UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
“Ni wakati wa kupiga kengele ya dharura”, amesema Katibu Mkuu wa UN katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa siku chache kabla ya kuanza kwa Mjadala wa Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akihojiwa na Assumpta Massoi wa UN News, António Guterres amegusia ushirikiano wa kimataifa, harakati za utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 duniani, mabadiliko ya tabianchi, usawa wa jinsia, viijana, amani na usalama barani Afrika na duniani kwa ujumla.