Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA 76 using tag UNGA76

MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
21 Septemba 2021-27 Septemba 2021

Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, #UNGA76 umefunguliwa Jumanne ya tarehe 14 mwezi Septemba mwaka 2021 kwenye makao makuu jijini New  York, Marekani. Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu utaanza Jumanne ya tarehe 21 mwezi Septemba mwaka 2021 na kumalizika tarehe 27 mwezi Septemba 2021. Katika ukurasa huu utapata taarifa motomoto kuhusu mjadala huo mkuu wa ngazi ya juu na matukio mengine ikiwemo miaka ufadhili kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi, mifumo ya chakula, maadhimisho ya miaka 20 ya azimio la Durban linalopinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zingine zote, mabadiliko ya tabianchi na ulinzi na usalama, masuala ya nishati  na pia kuenziwa kwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld.Vikao vingine vya ngazi ya juu vitakavyofanyika wakati wa wiki za mwanzo za #UNGA76 ni pamoja na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu COVID-19.  UNGA76 inafanyika wakati  janga la COVID-19 likiendelea kwa hiyo vikao vitafanyika moja kwa moja ukumbini makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini pia kwa njia ya mtandao ambapo baajhi ya wakuu wa nchi na serikali hotuba zao zitakuwa kititolewa kwa njia ya mtandao.

Tufuatilie katika majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

YouTube: https://www.youtube.com/c/UNNewsKiswahili

Twitter: https://twitter.com/HabarizaUN

UN Photo/Evan Schneider

Mjadala Mkuu wa UNGA76 wafungua pazia New York

Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 leo umeng’oa nanga rasmi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani ukifanyika moja kwa moja na pia kupitia mtandaoni ukiwaleta pamoja nchi 193 wanachama wa Umoja huo.

Flora Nducha na taarifa zaidi 
Abdullah Shahid Rais wa Baraza Kuu akifungua mjadala huo ambao umebeba mada ya “Kujenga mnepo kupitia tumaini la kujikwamua kutoka kwa janga la COVID-19,  kushughulikia mahitaji ya sayari dunia, kuheshimu haki za watu, na kuufufua Umoja wa Mataifa. " 

Sauti
4'52"

Jarida 21 Septemba 2021

Leo tarehe 21 Septemba mwaka 2021 ni siku ya amani duniani halikadhalika siku ya kwanza ya mjadala mkuu wa mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya UN nchini Marekani.
Karibu Usikilize Jarida ambapo utasikia mengi kuhusu #UNGA76

Sauti
17'16"
Rais Mteule wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdulla Shahid akiwa ndani ya  ukumbi wa Baraza hilo
UN/Eskinder Debebe

Licha ya magonjwa na uharibifu, Rais mteule wa Baraza Kuu asema matumaini ndio msingi wa ushindi

Mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unafungwa rasmi hii leo na kutoa fursa ya kufunguliwa kwa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA76 unafungua pazia lake hii leo huku rais wake mteule Abdulla Shahid kutoka Maldives akisema tumaini ndio limesalia kuwa tegemeo kwa mabilioni ya watu duniani wakati huu wakihaha katikati ya janga la COVID-19, uharibifu wa mazingira, vita na majanga mengineyo.

Sauti
3'15"
UN /Manuel Elias

Tanzania yawa Makamu wa Rais UNGA76 na mjumbe wa ECOSOC

Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA utakaoanza tarehe mosi mwezi Septemba mwaka huu. 

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Profesa Kennedy Gastorn, uchaguzi huo umefanywa na nchi wanachama, siku ya Jumatatu Mei 7, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa makamu marais 9 wa mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa mkutano huo wa 76 Abdulla Shahidi kutoka Maldives. 

Uchaguzi huo pia ulifanyika kumchagua Bwana Shahidi ambaye alimshinda mpinzani wake kutoka Afghanistan. 

Sauti
1'38"