Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA 76 using tag UNGA76

MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
21 Septemba 2021-27 Septemba 2021

Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, #UNGA76 umefunguliwa Jumanne ya tarehe 14 mwezi Septemba mwaka 2021 kwenye makao makuu jijini New  York, Marekani. Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu utaanza Jumanne ya tarehe 21 mwezi Septemba mwaka 2021 na kumalizika tarehe 27 mwezi Septemba 2021. Katika ukurasa huu utapata taarifa motomoto kuhusu mjadala huo mkuu wa ngazi ya juu na matukio mengine ikiwemo miaka ufadhili kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi, mifumo ya chakula, maadhimisho ya miaka 20 ya azimio la Durban linalopinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zingine zote, mabadiliko ya tabianchi na ulinzi na usalama, masuala ya nishati  na pia kuenziwa kwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld.Vikao vingine vya ngazi ya juu vitakavyofanyika wakati wa wiki za mwanzo za #UNGA76 ni pamoja na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu COVID-19.  UNGA76 inafanyika wakati  janga la COVID-19 likiendelea kwa hiyo vikao vitafanyika moja kwa moja ukumbini makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini pia kwa njia ya mtandao ambapo baajhi ya wakuu wa nchi na serikali hotuba zao zitakuwa kititolewa kwa njia ya mtandao.

Tufuatilie katika majukwaa yetu ya mtandao wa kijamii

YouTube: https://www.youtube.com/c/UNNewsKiswahili

Twitter: https://twitter.com/HabarizaUN

Jarida 22 Septemba 2021

Ikiwa leo ni Jumatano  tarehe 22 Septemba 2021 siku ya pili ya mjadala mkuu wa mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa #UNGA76 karibu kusikiliza jarida ambapo kubwa utakalo sikia leo ni miaka 20 baada ya azimio la Durban kuhusu kupinga ubaguzi hali ipoje?. Utasikia mahojiano mbalimbali kutoka nchini Kenya na Tanzania. 

 

Sauti
14'20"
Ann Sophie Persson

Dkt. Getrude Mongella azungumzia ubaguzi wa rangi

Wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 76, leo likijikita na mjadala wa ngazi ya juu kuadhimisha miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio la Durban linalopinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zingine, imeeldezwa kwamba hatua zimepigwa katika kupambana na ubaguzi wa rangi lakini bado kuna kibarua kigumu cha kufikia lengo la kutokomeza kabisa ubaguzi huo katika Nyanja mbalimbali.

Sauti
3'35"
Balozi Getrude Mongela ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa mkutano wa kimataifa wa 4 wa wanawake uliofanyika Beijing, China miaka 25 iliyopita.
UN Tanzania

Hakuna aliye na haki ya kumbagua mwingine sababu ya rangi yake:Mongella

Wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 76 #UNGA76 leo likijikita na mjadala wa ngazi ya juu kuadhimisha miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio la Durban linalopinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zingine, imeelezwa kwamba hatua zimepigwa katika kupambana na ubaguzi wa rangi lakini bado kuna kibarua kigumu cha kufikia lengo la kutokomeza kabisa ubaguzi huo katika Nyanja mbalimbali.

Sauti
3'35"
Rais wa Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la UN
UN/Cia Pak

Afrika imejipanga kujinasua na COVID-19 lakini uhisani uongezeke- Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo, ni miongoni mwa viongozi waliohutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 siku ya Jumanne ambapo amesema bara la Afrika tayari lina mkakati dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 lakini kinachohitajika sasa ni ufadhili wa fedha ili uchumi wao uweze kukwamuka.