Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waziri Mkuu wa Haiti anataka suluhisho la kudumu kwa shida ya uhamiaji 

Waziri Mkuu wa Haiti  Ariel Henry akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu, UNGA76
UN Photo/Cia Pak
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu, UNGA76

Waziri Mkuu wa Haiti anataka suluhisho la kudumu kwa shida ya uhamiaji 

Masuala ya UM

Wakati wa hotuba yake kwenye mjadala mkuu wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumamosi , waziri mkuu wa serikali ya Haiti, Ariel Henry, ametaka suluhisho la kudumu lipatikane kwa changamoto ya uhamiaj, akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuboresha haraka hali ya maisha katika nchi zinazotoa wakimbizi wa kisiasa au kiuchumi. 

Katika siku za hivi karibuni, waziri mkuu huyo alisema, "Taswira za njinsi ya wenzangu kadhaa wanavyotendewa kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani zimeshtua sana". 

Bila kupinga haki ya serikali yoyote ya huru wa kudhibiti kuingia kwa wageni ndani ya eneo lake au kuwarudisha kwenye nchi yao ya asili wale ambao wanaingia kinyume cha sheria, alitaka kukumbusha kwamba nchi kadhaa "zilizofanikiwa leo zilijengwa na mfululizo wa kuingia kwa mawimbi ya wahamiaji na wakimbizi ”. 

Uhamiaji utaendelea maadamu kuna maeneo yenye ustawi katika sayari yetu, wakati kuna sehemu kubwa ya idadi ya watu ulimwenguni wanaishi katika hali ya hatari na duni, wakati mwingine iliyokithiri, bila matarajio ya maisha bora, ameonya Bwana Henry. 

Kurejea kwa utendaji wa kawaida 

 Bwana Henry amekaribisha kaulimbiu ya matumaini iliyochaguliwa kwa kikao hiki cha 76, huku akisistiza kwamba "mshikamano na ushirikiano tu miongonim mwa watu ndio utakaowezesha kushinda janga la COVID-19, ambalo linaweka nchi zote, pamoja na yake, kuwa katika hali ngumu.” 

Waziri Mkuu pia amezungumzia hatua yake ya kuwa kiongozi wa Serikali, ambayo aliikubali muda mfupi kabla ya mauaji ya Rais Moïse. Ameonesha kuwa kipaumbele chake ni kuruhusu nchi kurudi katika utendaji wa kawaida "wakati karibu taasisi zote za kidemokrasia hazipo tena au hazifanyi kazi kabisa". 

Akitambua kuwa mazungumzo pekee na vyama vya kisiasa na wahusika wa asasi za kiraia ndio yatakayoweza kuleta muafaka wa kutosha kuhakikisha utulivu wa kijamii na kisiasa ametaja kufanya mikutano na majadiliano na sekta zote za jamii, maisha ya kitaifa, kwa lengo la kuandaa uchaguzi mkuu wa kuaminika, ulio uwazi na shirikishi haraka iwezekanavyo. 

Kwa Bwana Henry, "makubaliano mapya ya kisiasa ya utawala wa amani na ufanisi wa kipindi cha mpito ni hatua muhimu katika mchakato wa kurudisha utawala wa sheria na taasisi za kidemokrasia.” 

Lakini, amesema yuko tayari kuendelea na majadiliano ili kupanua wigo wa makubaliano na kupata msaada wa watu wengine kwa mradi huu wa kawaida. 

Majanga ya asili 

Mbali na mzozo wa kisiasa unaoathiri Haiti, matokeo ya majanga ya asili yanayorudia rudia, amekumbusha Bwana Henry, kwamba baada ya tetemeko la ardhi la 2010 na Kimbunga Mathew cha 2016, tetemeko la ardhi lenye nguvu, la Agosti 14 mwaka huu liliharibu rasi nzima kusini mwa nchi hiyo. 

Janga hilo liliacha watu wasiopungua 2,207, wakipoteza maisha , 344  hawajulikani waliko na zaidi ya 12,268 walijeruhiwa, wakati maelfu ya nyumba zilibomoka au kuharibiwa, pamoja na hospitali, shule, makanisa, madaraja na barabara, amesema waziri Mkuu huyo ambaye ambaye amesifu "kuongezeka kwa hiari kwa mshikamano wa jamii ya kimataifa. 

Zaidi ya mahitaji ya haraka ya kibinadamu, ametoa wito wa kuendelea kusaidia Haiti katika mchakato wa ujenzi mpya. 

"Tunahitaji kujenga vyema zaidi na kwa mnepo zaidi ili kuhimili hatari za mabadiliko ya tabianchi", amesihi waziri mkuu, ambaye kwake ni muhimu pia kurudisha uchumi na kuvutia uwekezaji wa kitaifa na nje. . 

"Idadi kubwa ya watu wetu ni vijana, wanahitaji kazi nzuri na matarajio bora," amesema Bwana Henry, ambaye amehitimisha kwa kutoa wito wa kuwa na mshikamano wa kimataifa wenye nguvu wakati wote. 

Shukran 

 Mwanzoni mwa hotuba yake, waziri mkuu wa Haiti ameushukuru tena Mkutano wa Baraza Kuu kwa  Julai 14 kumuenzi  Matrehemu Rais Jovenel Moïse, aliyeuawa wiki moja kabla ya tarehe hiyo. 

Amesisitiza azma yake ya kufanya kila linalowezekana kupata wahusika, washirika na wafadhili wa "uhalifu huo mbaya", na kuongeza kuwa Haiti iliomba msaada wa kisheria.