Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maldives yachaguliwa kuwa Rais wa UNGA76

Volkan Bozkir (cKatikati),Rais wa kikao cha 75 cha Baraza Kuu akisalimiana na Abdulla Shahid waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Maldives na Rais mteule wa Baraza Kuu kikao cha 76
UN Photo/Loey Felipe
Volkan Bozkir (cKatikati),Rais wa kikao cha 75 cha Baraza Kuu akisalimiana na Abdulla Shahid waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Maldives na Rais mteule wa Baraza Kuu kikao cha 76

Maldives yachaguliwa kuwa Rais wa UNGA76

Masuala ya UMLeo raia wa Maldives Abdulla Shahid amechaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Rais wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja huo au UNGA76.

Katika kinyang’anyiro hicho nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamelazimika kuchagua kati ya wagombea wawili wanaowakilisha nchi mbili kutoka kwa kundi la mataifa ya Asia-Pacific: Afghanistan na Maldives. Walnachama hao wakampendekeza waziri wa mambo ya nje wa Maldives Abdulla Shahid kumwacha mpinzani wake ambaye ni mkuu wa zamani wa diplomasia wa Afghanistan, Zalmai Rassoul.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Rais wa sasa wa Baraza Kuu, Volkan Bozkir, wamempongeza Bwana Shahid kwa uchaguzi huu.
"Kama chombo kinachowakilisha zaidi, Baraza Kuu ndio nguzo ya kazi zetu zote katika Umoja wa Mataifa na ni chombo muhimu kwa ufanisi wetu kama Shirika. Mwaka 2021, ulimwengu unahitaji ufanisi huu zaidi ya hapo awali," amesema na kusisitiza Bwana Guterres.
Katibu Mkuu na Rais wa Mkutano Mkuu wamesifu uzoefu mkubwa wa kidiplomasia wa Bwana Shahid. 
Akiwa na umri wa miaka 59, Bwana Shahid amewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Maldives mara mbili (mnamo mwaka 2007-2008 na tangu 2018 hadi sasa), uzoefu ambao "unampa ufahamu wa kina juu ya umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabili changamoto za ulimwengu leo," ameongeza kusema Bwana.Guterres 

Abdulla Shadidi wa Maldives akipanda jukwaani kwenye ukumbi wa Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa kikao cha 76 cha Baraza hilo
UN Photo/Loey Felipe
Abdulla Shadidi wa Maldives akipanda jukwaani kwenye ukumbi wa Baraza Kuu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa kikao cha 76 cha Baraza hilo

Sauti imara kwa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea 

Kwa upande wake Rais wa sasa wa Baraza Kuu Bozkir amekumbusha kuwa Bwana Shahid "amekuwa sauti imara kwa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea".
Kisiwa kilicho na visiwa vingine vidogo 26 katika Bahari ya Hindi, Maldives inashughulikia eneo la kilomita za mraba 298 na eneo la bahari karibu kilomita za mraba 90,000, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi zilizo na wilaya zilizotawanywa zaidi duniani. 

Nchi hiyo inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikilazimika kupambana na kina cha bahari kujaa hali inayotishia uwepo wa visiwa vyake.
"Akitoka katika kisiwa kidogo kinachoendelea, Bwana Shahid ataleta ufahamu wa kipekee kwenye kikao cha 76 cha Baraza Kuu, tunapojiandaa kwa mkutano waUmoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi huko Glasgow mwezi Novemba", amesisitiza Bwana Guterres.

Katibu Mkuu pia amefafanua kuwa kikao cha 76 cha MBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambacho kitaanza Septemba, kitashughulikia athari za janga hilo kwenye nguzo tatu za kazi yetu ambazo ni amani, maendeleo endelevu na haki za binadamu. 
Kwa niaba ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu amemtakia Bwana Shahid kika mafanikio na kumpongeza "kwa kuchagua matumaini kama mada kuu" ya maono ya urais wake ujao.

Nchini Maldives, Bwana Shahid pia alikuwa  mwanasiasa ambayo ilishuhudia akichaguliwa kama mbunge na kisha spika wa bunge la Maldives. 
Rais ajaye wa Baraza Kuu ana shahada ya uzamili (BA) katika masuala ya Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Canberra cha Elimu ya Juu, nchini Australia, na ana stashahada ya uzalimi (MA) katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa kutoka Shule ya Sheria na Diplomasia ya Fletcher katika Chuo Kikuu cha Tufts, huko nchini Marekani..