Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Rais wa Baraza Kuu, Abdulla Shahid akihutubia kwenye kongamano la biashara wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola, moja ya kando ya Mkutano wa Wakuu wa Serikali za Jumuiya ya Madola, mjini Kigali, Rwanda.

Rais wa Baraza Kuu la UN, aitumia CHOGM kupeleka ujumbe mzito

UN PGA
Rais wa Baraza Kuu, Abdulla Shahid akihutubia kwenye kongamano la biashara wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola, moja ya kando ya Mkutano wa Wakuu wa Serikali za Jumuiya ya Madola, mjini Kigali, Rwanda.

Rais wa Baraza Kuu la UN, aitumia CHOGM kupeleka ujumbe mzito

Tabianchi na mazingira

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdulla Shahid yuko katika mji Mkuu wa Rwanda Kigali ambako unafanyika Mkutano wa 26 wa wakuu wan chi za Jumuiya ya Madola.

Bwana Shahid ameanza programu yake rasmi na hotuba katika tukio la ngazi ya juu kuhusu "Kuweka 1.5 Hai" liliyoandaliwa na Rwanda na Uingereza kandoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola, CHOGM 26. Akihutubia mkutano huo, ambao ni kwa mara ya kwanza Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwahi kuhuhudhuria, Bwana Shahid amesisitiza kuhusu kuendelea kupamabana na mabadiliko ya tabianchi akisema, “tuna uwezo wa kutimiza ahadi zetu zote za tabianchi. Tuna ueledi, tuna rasilimali, na tuna teknolojia. Tunaweza kuhamia vyanzo vya nishati mbadala, tunaweza kupunguza hewa chafuzi, na tunaweza kuhifadhi dunia yetu na mifumo yake ya ikolojia. Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.” Ameongeza akisema, “juhudi hizi lazima ziwe sehemu ya juhudi zetu za muda mrefu za kupunguza utoaji wa hewa ukaa, na kuleta msukumo tunapoangazia COP27 huko Sharm El-Sheikh, Misri.” Amesema kaulimbiu ya CHOGM ya mwaka huu sio tu imeendana na wakati, bali pia ni yani yenye umuhimu wa haraka. Kaulimbiu ya mkutano huo ni Kuwasilisha mstakabali wa pamoja: Kuunganisha, Kubuni, Kubadilisha, kwa kuzingatia "Kuurekebisha Ulimwenguni". Akisisitiza, kiongozi huyo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ameeleza kuwa wakati dunia wakati dunia inaendelea kukabiliana na athari na juhudi za kujenga upya baada ya janga la COVID-19, janga la tabianchi linaendelea bila kupunguzwa na hivyo “tunahitaji masuluhisho kwa dharura ikiwa tunataka kufikia malengo yetu na kutimiza ahadi zetu, sio tu kwa kila mmoja wetu bali kwa vizazi vijavyo pia.” Wanawake Rais Shahid pia amepata fursa ya kuzungumza katika tukio jingine la kandoni mwa CHOGM 26 lililohusu kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake, liliyoandaliwa na Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame. Amebainisha kuwa kukomesha ubaguzi wa kijinsia na unyanyasaji ni kipaumbele cha kimataifa ambacho kinahitaji hatua za haraka za pamoja. Na hatua hiyo inahitaji kuwiana na kujumuishwa katika “kupona kwetu kutoka katika sera za Covid-19.” Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana sio tu ni ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unaimarisha usalama na usalama wa wahasiriwa wake, “lakini pia unazuia nafasi za wanawake na wasichana kuwa washiriki kamili na sawa katika jamii.” Amesema. Kongamano la biashara Ushiriki wake wa tatu ulikuwa kwenye kongamano la Biashara la Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola, likilenga kupona kutokana na COVID. Amelitumia tukio hilo kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuharakisha hatua za Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG ili kujenga upya kwa ubora, imara, kijani kibichi na buluu. “Janga hili limetuonyesha kuwa sayansi na uvumbuzi ndio kiini cha juhudi hii ya kubadilisha ulimwengu wetu kuwa bora na kufikia Ajenda yetu ya 2030.” Amesema.