Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nguvu ya ubinadamu inaweza kushinda COVID-19, changamoto za mabadiliko ya tabianchi: Shahid

Rais wa Baraza Kuu Abdulla Shahid akihutubia katika Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76
UN Photo/Cia Pak
Rais wa Baraza Kuu Abdulla Shahid akihutubia katika Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76

Nguvu ya ubinadamu inaweza kushinda COVID-19, changamoto za mabadiliko ya tabianchi: Shahid

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo amefungua mjadala wa ngazi ya juu wa kila mwaka, ambao mwaka huu umefanyika kupitia mtandao na wajumbe wengine zaidi ya 100 kushiriki ana kwa ana ukumbini,

Kwneyehotuba yake amekumbuka siku zenye giza za janga la Corona au coronavirus">COVID-19, "wakati miji ilipokuwa imefungwa na chanjo bado ni ndoto" na jinsi gani watu wa dunia "walikusanyika pamoja kuliko kuliko wakati mwingine wowote". 

Abdulla Shahid kutoka Maldives amesema kuwa baada ya mwaka mmoja na nusu wa mateso ya upweke na wasiwasi , ilikuwa ni matumaini na hali ya ubinadamu wa pamoja iliyowezesha kukutana tena huku, na kuongeza kwamba "Wacha tuwape matumaini sasa". 

Alikumbusha kwamba katika muda uliovunja rekodi, wanasayansi walishirikiana ulimwenguni koyte kutengeneza chanjo nyingi za COVID-19 na chanjo kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya wanadamu akiita "jukumu kubwa la kujivunia". 

 Kukosa usingizi 

Rais huyo wa Baraza Kuu amesema kuwa katika miezi 12 ijayo, ulimwengu unataka suluhisho kwa changamoto za pamoja za "udhaifu, mizozo, COVID-19, na mabadiliko ya tabianchi. Masuala haya huwafanya raia wetu kuwa macho usiku kucha, husababisha wasiwasi wa pamoja na wasiwasi kwamba mambo yanazidi kuwa mabaya na wako sahihi kwani tunaweza kufanya juhudi zaidi.”  

Wanawake wakishiriki kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi nchini Bangladesh
UNDP Bangladesh
Wanawake wakishiriki kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi nchini Bangladesh

Mchanganuo wa masuala muhimu 

Kwenye suala la COVID-19, afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameelezea kuwa ulimwengu una chanjo, ujuzi na uwezo wa usambazaji, lakini "tunakosa msaada wa kisiasa tu". 

Na licha ya ubunifu mpya wa nishati mbadala, teknolojia inayoweza kubadilika, na kubadilisha mwelekeo kutoka kwa mafuta kisukuku na kuingia kwenye nishati safi, msaada wa kisiasa na ufadhili unaohusiana unakosekana katika mazingira haya yanayobadilikabadilika. 

Wakati akiangazia hamu ya dunia ya kutaka kutokomeza na upokonyaji wa silaha za nyuklia, Rais wa Baraza Kuu amesema, "bado tunakwama kwenye mstari wa kumalizia, na kuacha mikataba bila kuridhiwa". 

Hatimaye, kwa upande wa masuala ya kibinadamu, amesema kuwa licha ya kuwa na chakula na maji ya kutosha ulimwenguni, bado njaa na ukame hutegemea vinatamalaki. "Mamia ya mamilioni ya watu watahitaji msaada wa kibinadamu kuelekea mwishoni mwa mwaka", ameonya Bwana Shahid. 

Wakati wa kufuata njia mpya 

Bwana Shahid akionyesha kuwa tunaishi wakati wa mabadiliko amesema "Tunaweza kuchagua njia ya kujiteng kuangamizana ... kuhama polepole kwa jaribio la wanadamu, au tunaweza kufuata njia mpya, endelevu na njia thabiti inayobadilisha mustakbali wa sayari yetu ”. 

Wakati akilielezea janga la COVID-19 kama "janga la kiwango kikubwa zaidi", amelitaja pia kama ni "upenyo katika mgodi wa makaa ya mawe", akionya juu ya hatari ambazo ziko mbele endapo uchaguzi mgumu lakini muhimu hautafanyika. 
Bwana Shahid amesema nguvu ya ubinadamu inaweza kushinda changamoto na kwamba ana matumaini "kwamba tunaweza kuzipita itifaki na vizuizi vya kubadilisha jamii zetu". 
Mionzi ya matumaini 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ametanabaisha nia yake ya kufuata "miale ya matumaini" mitano wakati akiongoza kikao cha 76 Baraza Kuu, akianza na usawa wa chanjo. 

Katika hilo amesema antaandaa mkutano wa ngazi ya juu utakaojikita kuangalia vikwazo vya usambazaji, uhifadhi na mgawanyo. 
Na kuhusu kujikwamua vyema na kwa muda mrefu wa dhidi ya COVID-19, ameapa kushinikiza kujijenga "mnepo bora, wa nguvu, na kwa kujali mazingira kwa kufuata njia zilizowekwa na Ajenda 2030 ya maendeleo endelevu kwa wote tunaweza kujitenga na mazoea mabaya na kukumbatia maisha bora ya baadaye",  

Mabadiliko ya tabianchi yameongeza hatari ya hali ya hewa kavu, ya joto ambao inachangia kuchochea moto wa nyika
Unsplash/Mikhail Serdyukov
Mabadiliko ya tabianchi yameongeza hatari ya hali ya hewa kavu, ya joto ambao inachangia kuchochea moto wa nyika

Mabadiliko ya tabianchi 

Rais wa Baraza Kuu ameelezea umuhimu wa kuzingatia tena changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, "ambayo imewekwa kando sababu ya COVID-19". 

Akinukuu ripoti ya jopo la serikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi (IPCC), amesema: "Hatuko tena kwenye njia mbaya tuko kwenye ncha ya mwamba". 

Ili kushughulikia hili, Bwana Shahid atakuwa mwenyeji wa hafla kadhaa za hatua za mabadiliko ya tabianchi, akianza na kusaidia kuziba mapengo ili kutimiza ahadi za mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Novemba wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Scotland (COP26), na baadaye, "Mkutano wa mazingira” ambayo inajumuisha masuala yanayofungamana ya bahari, jangwa na viumbe hai.” 

Kuzingatia ufanisi 

Mwishowe, Rais wa UNGA76 amesisitiza umuhimu wa kuendelea kwa mageuzi na ufufuaji wa Umoja wa Mataifa, akisema "hii sio juu ya uwiano wa nguvu, hii ni juu ya ufanisi". 

"Hatujawahi kuimarika sana kiteknoloji, kushikamana au kuwa na utajiri, rasilimali, au ujuzi ambao tunao sasa. Hakuna kitu katika njia yetu cha kutuzuia isipokuwa sisi wenyewe. Tuwe Umoja wa Mataifa ambao watu wanautaka ”, amesema.