Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

© UNICEF/Andrew Brown

Ukame Turkana Umeathiri elimu, UNICEF yahaha kusadia watoto kusalia shuleni

Ukame unaoendelea Pembe ya Afrika umeathiri shule zaidi ya 100 katika kaunti ya Turkana Kenya na kusababisha watoto wengi kuacha shule. Sasa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya kwa ushirikiano na mradi wa Educate a Child wanaisaidia serikali kusajili watoto shuleni na kuhakikisha waliosajiliwa wanasalia shuleni.

"Niliacha shule nikaenda mitaani, Maisha mitaani yalikuwa magumu sana, njaa kila siku na nilikosa mahali pa kula na kulala.”

Sauti
2'41"
FAO

Jamii Somaliland zasaidiwa kupambana na uhaba wa chakula: FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linaendesha mradi wa miaka minne wa mnepo wa uhakika wa upatikanaji wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na migogoro pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi katika pembe ya Afrika lengo likiwa ni kujenga amani na kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo.

Video ya FAO ikimuonesha Asha Mohammed Ali mama wa watoto 8 na mkulima kutoka wilaya ya Wadaamago huko Somaliland akiwa shambani anapalilia mazao yake huku akisimulia namna ukame ulivyowaathiri wakulima na kuharibu kabisa mustakabali wa maisha yao.

Sauti
1'45"
Wanufaika wa miradi inayotekelezwa na FAO nchini Somalia
©FAO/Arete/Ismail Taxta

Uwekezaji wa kimkakati unahitajika ili kuboresha uhakika wa chakula na maji kwa mamilioni ya Wasomali

Wakati misaada ya kibinadamu imesaidia baadhi ya maeneo ya Somalia kutotumbukia kwenye baa la njaa, wananchi wa vijiji nchini humo bado wanaendelea kukabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO hii leo baada ya hivi karibuni kutangazwa matokeo ya uchunguzi wa uhakika wa chakula.