Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Mandhari ya milima mjini Sharm El-Sheikh, na Qesm Sharm Ash Sheikh, Misri
Unsplash/Juanma Clemente-Alloza

COP27: Unachohitaji kufahamu kuhusu mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa la mwaka huu.

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu unafanyika huko Sharm el-Sheikh,nchini Misri wakati ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.

Mama amempeleka mwanye aliyeathirika vibaya na utapiamlo kwenye kituo cha lishe cha WFP Torit nchini Sudan Kusini
© WFP/Eulalia Berlanga

Mabadiliko ya tabianchi yazidisha zahma ya utapiamlo na njaa Sudan Kusini:UNICEF/FAO/WFP 

Umoja wa Mataifa umeonya hii leo kuwa njaa na utapiamlo vinaongezeka katika maeneo yote yaliyokumbwa na mafuriko, ukame na mizozo nchini Sudan Kusini huku baadhi ya jamii zikiwa hatarini kukumbwa na njaa iwapo misaada ya kibinadamu haitakuwa endelevu, halikadhalika mikakati ya kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi haitaimarishwa. 

13 OKTOBA 2022

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Dunia ipo hatarini kuingia katika mwaka mwingine wenye uhaba wa chakula wakati huu ambapo watu wengi tayari wanazidi kuingia katika dimbwi la uhaba wa chakula, limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP ambalo limetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kushughulikia mzizi wa tatizo hili wakati dunia ikielekea kuadhimisha siku ya chakula duniani hapo Oktoba 16.

Sauti
12'35"

11 OKTOBA 2022

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Umoja wa Mataifa umeshtushwa na ongezeko kubwa la wakimbizi wa ndani huko magharibi kwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC baada ya kuibuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwezi Julai huko Kwamouth.

Sauti
10'44"
Csaba Kőrösi  Rais wa UNGA77 akiendesha mjadala wa wazi wa Baraza Kuu katika siku ya mwisho ya mjadala huo
UN Photo/Cia Pak

Körösi, akunja jamvi la mjadala wa ngazi ya juu wa UNGA77

Magari yaliyotanda kuzunguka makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wakati wa wiki ya mjadala wa ngazi ya juu wa viongozi kwenye Baraza Kuu UNGA77 sasa yameondoka na barabara iliyofungwa kufunguliwa, polisi wengi na maafisa wa ujasusi ambao walizuia njia za kuelekea kwenye jengo la Umoja wa Mataifa, nao wametrejea kwenye majukumu yao ya kila siku, kilomita za vyuma vilivyokuwa vizuizi kuzunguka eneo hilo la Umoja wa Mataifa New York, vinavyojulikana kama Turtle Bay navyo vimesafirishwa kwa malori hadi kwenye maghala kusubiri hadi mwakani kwani wiki ya mjadala wa ngazi ya juu imemalizika kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  .

Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mambo ya Nje wa India, akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu.
UN Photo/Cia Pak

Vita ya Ukraine na Urusi: India iko upande wa amani na itasalia huko

India imesema itaendelezeka ahadi zake za ushirikiano wa pande nyingi, wenye ushahidi uliothibitishwa,  uamuzi wa kusambaza chanjo kwa mataifa zaidi ya 100 duniani, kutoa misaada ya maafa kwa wale walio katika taabu, kushirikiana na nchi nyingine, kwa kuzingatia ukuaji wenye kujali mazingira, muungano bora wa kidijitali na upatikanaji wa huduma ya afya.