Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa ni nini na kwa nini ni muhimu?
Umewadia wakati ambapo nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zitapata fursa ya kuonesha kwamba vitendo vya mazingira vinaweza kuunganisha ulimwengu. Wakati huu ni Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira, au Unea, ambalo mkutano wake wa sita utafanyika kati ya Februari 26 na Machi 1, 2024 Nairobi, Kenya.
Mkutano wa Baraza la Mazingira Duniani UNEA6 wangoa nanga Nairobi Kenya
Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya. Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.