Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Habari kwa ufupi:
Mkutano wa kimataifa kuhusu Gaza wafanyika jijini Paris Ufaransa, FAO inakabiliana na changamoto ya El Niño kwa wakulima na WHO kujenga mifumo ya afya yenye mnepo
UNCCD kujengea mnepo jamii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi Kenya
Shirika la Umoja wa mataifa la kudhibiti ueneaji wa majangwa, UNCCD, liko mstari wa mbele kushirikiana na jamii kupata mbinu za kujenga mnepo dhidi ya madhila ya mabadiliko ya tabia nchi.
UNICEF na wadau wake wabuni mbinu za kukabiliana na janga la tabianchi na changamoto katika jamii nchini Kenya
Janga la tabianchi limesababisha kupotea kwa upatikanaji wa elimu, huduma muhimu, na ajira kwa vijana nchini Kenya, hata hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini humo kwa kushirikiana na shirika la Equal Access International wanawawezesha vijana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko tabianchi na kutoa ufahamu kuhusu suluhisho la kukabiliana na tatizo hilo.
UNICEF na Equal Access International, wabuni mbinu za kukabiliana na changamoto katika jamii
Janga la tabianchi limesababisha kupotea kwa upatikanaji wa elimu, huduma muhimu, na ajira kwa vijana nchini Kenya. Hata hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Equal Access International wamewawezesha vijana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa ufahamu kuhusu suluhisho la kukabiliana na tatizo hilo. Evarist Mapesa wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anatufafanulia zaidi katika Makala hii.
11 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati, na mradi wa maji Baringo nchini Kenya. Makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya 10 ya tamko la haki za binadamu na mashinani tunamulika siku ya mtoto wa kike duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 kila mwaka ambayo ni leo.
Nchi zilizo katika bonde la mto Nile kunufaika na mradi wa tahadhari za mapema
Maji yakiwa mengi yanaweza kusababisha mafuriko kama yaliyotokea hivi karibuni huko nchini Libya na uwepo wa maji kidogo unaweza kusababisha ukame kama hali ilivyo kwa nchi nyingi za ukanda wa Jangwa la Sahara kwa sasa, na ndio maana wadau wa masuala ya hali ya hewa wametaka suala la maji kuwa kitovu wakati dunia inashughulikia mabadiliko ya tabianchi.
UN tuondoleeni vikwazo vya silaha - Rais Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini, Salvar Kiir Magardit, ametaka nchi yake kuondolewa vikwazo vya silaha akieleza vinakwamisha maendeleo ya nchi yao.
Tunaelimisha wanafunzi na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi - Madina Jubilate Kimaro
Wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania.
Muungano wa mabadiliko ya tabianchi wadai hatua, huku Guterres akionya Ubinadamu umefungua milango ya kuzimu
"Joto la kupindukia linaleta madhara ya kutisha duniani ", kwa mujibu wa mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akizungumza leo katika mkutano wa kwanza kabisa wa ngazi ya juu wa matarajio kuhusu mabadiliko ya tabianchi mbele ya mbele ya muungano wa kimataifa wa kuchagiza hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ulijumuisha wachagizaji, watendaji, wanasiasa, wafanyabiashara, mashirika ya kimataifa na viongozi wa asasi za kiraia waliokusanyika New York kandoni mwa mjadala wa Baraza kuu UNGA78.