Mabadiliko ya tabianchi yanaifanya dunia kutokalika aonya Guterres

Ubinadamu unakabiliwa na ukweli mchungu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelekea siku ya hali ya hewa duniani, itakayoadhimishwa kesho Ijumaa akionya kwamba uharibifu ambao tayari umesababishwa na mabadiliko ya tabianchi "unaifanya sayari yetu kutokalika”.
Ametoa changamoto kwa serikali ulimwenguni kote, kuufanya mwaka 2023 kuwa mwaka wa "mabadiliko, na sio mchezo" linapokuja suala la kushughulikia kwa umakini mabadiliko ya tabianchi, na hatua zenye mashiko za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema “Mabadiliko ya tabianchi yanazidisha mawimbi ya joto, ukame, mafuriko, moto wa nyika na njaa”. Ameonya hayo huku akisisitiza kwamba mabadiliko hayo yanatishia kuzamisha nchi na miji ya mabondeni huku viwango vya bahari vikiongezeka kutokana na kuyeyuka kwa barafu na hali ya hewa inayozidi kuwa mbaya.
Athari ya pamoja ya hii itakuwa kusababisha vioumbe vingi na mbalimbali kutoweka, amesema bwana Guterres.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya utabiri wa hali ya hewa ni, “Mustakabali wa hali ya hewa, hali ya hewa na maji katika vizazi na vizazi” na kaulimbiu hii “inatulazimisha sote kutimiza wajibu wetu kwa vizazi vijavyo,” ameongeza.
Guterres amesema "Hiyo inamaanisha kuharakisha hatua za kupunguza ongezeko la joto hadi kufikia nyuzi joto 1.5, kupitia hatua za kupunguza na kujenga mnepo. Inamaanisha kubadilisha kwa kiasi kikubwa mifumo yetu ya nishati na usafiri, kuvunja uraibu wetu wa nishati ya visukuku, na kukumbatia hatua za mpito wa haki wa kuelekea nishati mbadala.”
Amesema mataifa yaliyoendelea yana wajibu sasa wa kuongoza mapinduzi ya kifedha na kiufundi ambayo yanaweza kusaidia nchi zote kupunguza utoaji wa hewa ukaa, kujenga mnepo wa siku za usoni kwa kuingiza vyanzo vya nishati mbadala kama vile maji na upepo, na kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga yatokanayo na hali ya hewa.
Jambo kuu kati ya haya, Bwana Guterres amesema ni hitaji la dharura la kushughulikia hasara na uharibifu unaoathiri nchi ambazo haziwezi kustahimili na angalau kwa makosa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
"Na inamaanisha kuishi kulingana na ahadi iliyotolewa siku ya yali ya hewa duniani iliyotolewa mwaka jana ya kuhakikisha kuwa mifumo ya tahadhari ya mapema dhidi ya majanga ya mabadiliko ya tabianchi inamfikia kila mtu ulimwenguni. Nchi 30 sasa zimetambuliwa kuharakisha utekelezaji mwaka huu.”
Amehitimisha kwa kusema kuwa "Ni wakati wa kumaliza vita visivyokoma na visivyo na maana dhidi ya asili na kutoa mustakabali endelevu ambao mahitaji yetu ya hali ya hewa, na watoto wetu na wajukuu wanastahili."