Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko New zealand kwa vita dhidi ya silaha, chuki, na mabadiliko ya tabianchi:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri mkuu wa New Zealand mjini Aucland
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri mkuu wa New Zealand mjini Aucland

Heko New zealand kwa vita dhidi ya silaha, chuki, na mabadiliko ya tabianchi:UN

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterees yupo ziarani , Auckland, mjii mkuu wa New Zealand hii leo, ambapo kwenye mkutano wa  pamoja na Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden mbele ya waandishi wa habari amesisitiza ushirikiano wake na waathirika wa mashambulizi dhidi ya msikiti katika mji wa Christchurch mwezi Machi yaliyokatili maisha ya  watu 51 na kujeruhi wengi wengine.

UN social Media/Priscilla Lecomte
Dansi za kimaori zatamalaki ziara ya Guterres New Zealand

 

Katika hotuba yake Bw. Guterres  amesema kawaida hutoa“salamu za mshikamano”kwa nchi za Kiislamu wakati wa Ramadani lakini mwaka huu ameamua kutembelea jumuiya ya Kiislamu huko Christchurch, kutoa salamu za rambirambi kwa ujasiri wao, lakini pia kwa mshikamano wa ajabu na ujumbe wa umoja uliotolewa na serikali ya New Zealand.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia ametoa pongezi kwa hatua ya haraka aliyoichukuwa  Waziri Mkuu Arden na serikali baada ya tukio hilo, za kuimarisha sheria ya udhibiti wa silaha, na pia wito wa kuzuia hotuba za chuki kwenye vyombo vya habari  katika jamii na mitandaoni.

Guterres ameongeza pia hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Bi Arden kwamba ni muhimu sana katika mipango ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na hotuba za chuki, na kusaidia nchi kulinda maeneo matakatifu kama nyumba za ibada.

New Zealand katika vita vya tabianchi 

Ziara ya Katibu Mkuu New Zealand ni sehemu ya ziara yake katika  mataifa yaliyopo kwenye visiwa vya Pasifiki ambapo suala la dharura katika takwimu za mabadiliko ya hali ya tabianchi ni la msingi sana.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres akipewa salamu za kiasili baada ya kuwasili New Zealanda kabla ya kufanya mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri Mkuu wa nchi hiyo Jacinda Arden
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres akipewa salamu za kiasili baada ya kuwasili New Zealanda kabla ya kufanya mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri Mkuu wa nchi hiyo Jacinda Arden

Katika mkutano wake na  waandishi wa habari, Bw Guterres ameshukuru New Zealand katika juhudi zake za kuongoza mapambano dhidi ya dharura ya mabadiliko ya tabianchi na pia msaada kwa mataifa ya visiwa vya Pasifiki yanayokabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

"Nitatembelea Fiji, Tuvalu na Vanuatu natuma ujumbe kutoka visiwa vya Pasifiki kwenda dunia nzima. Ni dhahiri kwetu sote  kuwajibika, na ni lazima kuwa na uwezo kukabiliana na hali hii ambayo nimtihani na kuukabili. Hatuwezi kuruhusu hali ya kukimbizana na  mabadiliko ya tabianchi.Tunahitaji kulinda maisha ya watu wote na tunahitaji kulinda sayari yetu. "

Katibu Mkuu pia amezungumzia umuhimu wa kuanzishwa kwa sheria mpya ya New Zealand ya kupunguza kiwango cha hewa ukakaa kabla ya kufikia mwaka wa 2050, itakayosaidia kiwango cha nyuzi joto  kutozidi 1.5 mwishoni mwa karne hii, lengo lililorejelewa na jamii, wamesema wana sayansi katika ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwezi Oktoba 2018.

Hata hivyo, amesema dhamira ya kufikia mwafaka huo imeanza kupungua kwa baadhi ya nchi, ingawa wanafahamu umuhimu wa utendaji wao katika sual hilo, ambao ni moja ya sababu za kuzindua Mkutano maalum wa mabadiliko ya tabianchi katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York mwezi  Septemba  mwaka huu.