Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame Turkana Umeathiri elimu, UNICEF yahaha kusadia watoto kusalia shuleni

Ukame Turkana Umeathiri elimu, UNICEF yahaha kusadia watoto kusalia shuleni

Pakua

Ukame unaoendelea Pembe ya Afrika umeathiri shule zaidi ya 100 katika kaunti ya Turkana Kenya na kusababisha watoto wengi kuacha shule. Sasa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya kwa ushirikiano na mradi wa Educate a Child wanaisaidia serikali kusajili watoto shuleni na kuhakikisha waliosajiliwa wanasalia shuleni.

"Niliacha shule nikaenda mitaani, Maisha mitaani yalikuwa magumu sana, njaa kila siku na nilikosa mahali pa kula na kulala.”

Huyo ni Emmanuel Ekiru mwenye umri wa miaka 10 mmoja wa wanafunzi walioathirika katika kaunti hii ya turkana na kulazimika kuacha shule, ambapo takwimu za UNICEF zinaonyesha kwamba zaidi ya wanafunzi 22,200 wameathirika na ukame huo na karibu shule 40 hivi sasa hazina huduma za kutosha za maji safi na salama.

Ukame huo pia umesababisha hali ngumu ya maisha na kushindwa kujikimu kwa familia nyingi, Teresa Asinyen ni mama wa Emanuel anasema ili kukidhi mahitaji ya familia “ Imeniladhimu kusenya kuni na kuuza na pia kufanyakazi za ndani kwenye nyumba za watu. Natumia fedha ninazopata kulisha watoto wangu . Kulikuwa na ukame mbaya wati wa janga la COVID-19, na shule zilizpofungwa watoto walikwenda kusaka chakula, nilihaha kulisha watoto wangu na mara nyingi walijilisha wenyewe.”

Lakini sasa UNICEF kwa kushirikiana na mradi wa Educate a child au elimisha mtoto wanaisaidia serikali kurejesha shuleni watoto kama Emmanuel na kusajili wapya huku pia wakiwapa mlo shuleni .
Hadi kufikia sasa Watoto 157,000 wamefaidika na mradi huo akiwemo Emmanuel. Mwalimu Mary Ikay kutoka shule ya msingi ya Nakwamekwi ndiye aliyeenda kuzungumza naye, “Niliweza kukutana na Emmanuel nikajaribu kuzungumza naye kama mwanangu , nikamuuliza shida ilikuwa ni nini , ndipo nikaweza kumleta shuleni na mwalimu mkuu alichukua hatua kumsaidia, kuzungumza naye na kumpatia mahitaji ambayo hakuwa nayo ili aweze kuendelea na masomo na pia kumuingiza kwenye program yam lo shuleni.”

UNICEF inasema lengo ni kufikia watoto 48,000 walioacha shule na kuwarejesha shuleni katika kaunti nne ikiwemo Turkama, West Pokot, Baringo na Samburu.

Lakini kwa Emmanuel sasa mambo yamebadilika hata ana ndoto, “Nikienda shule sasa nafurahia masomo , nikiwa mkubwa nataka kuwa daktari"

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'41"
Photo Credit
© UNICEF/Andrew Brown