Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
La Ninã inatarajiwa baadaye mwaka huu lakini joto litasalia kuwa juu:WMO
Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO linatabiri kuongezeka kwa ukame katika baadhi ya maeneo duniani na kuongezeka kwa hatari ya mafuriko katika maeneo mengine.
Hali ya hewa, tabianchi au majanga ya maji yanaua kwa wastani watu 115 kila siku
Maafa yanayohusiana na hali ya hewa, tabianchi au majanga ya maji yalitokea katika miaka 50 iliyopita na kuua kwa wastani watu 115 kila siku na kusababisha hasara ya dola milioni 202 kila siku, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa hii leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO.
(Taarifa ya Moses Mghase)
Jarida Septemba 01 2021
Katika jarida na Grace Kaneiya hii leo utasikia ziara maalum ya Balozi Liberata Mulamula amaye ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania nchi Marekani kuzungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Pia utasikia taarifa inayoangazia ripoti mpya ya hali ya hewa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO
Mabadiliko ya tabianchi yanasabisha hali mbaya zaidi ya hewa lakini maonyo ya mapema yanaokoa maisha
Maafa yanayohusiana na hali ya hewa, tabianchi au majanga ya maji yalitokea katika miaka 50 iliyopita na kuua kwa wastani watu 115 kila siku na kusababisha hasara ya dola milioni 202 kila siku, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa hii leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO.
Kemikali ya risasi yaondolewa kwenye petroli duniani kote.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe wa pongezi kwa mshikamano wa serikali za nchi zinazoendelea, wafanyabiashara wakubwa na wananchi wa kawaida kwa juhudi zao za kutokomeza matumizi ya kemikali ya risasi katika mafuta ya petroli.
Watoto bilioni 1 wako hatarini kwa athari za mabadiliko ya tabianchi:UNICEF Ripoti
- Walio katika hatari zaidi ni kutoka Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Nigeria, Guinea, na Guinea-Bissau
- Mtoto 1 kati ya 3 ulimwenguni wanaishi katika maeneo ambayo angalau majanga manne ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira yapo au yanaingiliana.
- Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote wanaishi katika maeneo yaliyoathiriwa na majanga makubwa matano.
Jarida 20 Agosti 2021
Hii leo katika jarida utasikia mahojiano na manusura wa Covid-19, Bwana Ole Pertet, mmoja wa wakazi wa Marekani waliougua mwanzoni kabisa ugonjwa huo ulipoingia Marekani.
Lakini kabla ya mada hiyo utasikia habari kwa ufupi ambapo kuelekea siku ya kimataifa ya kumbukumbu na kuwaenzi waathirika wa ugaidi, itakayoadhimishwa hapo kesho Agost 21, leo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu kuwaenzi waathirika hao ukijikita zaidi katika msaada wa kisaikolojia na ulinzi kwa waathirika.
Wahudumu wa kibinadamu wahatarisha maisha yako kila uchao kuokoa ya wengine:Guterres
Leo ni siku ya wahudumu wa masuala ya kibinadamu duniani ambao wako msitari wa mbele kusaidia kuokoa maisha ya watu walio hatarini zaidi duniani majanga yanapozuka, na kwa kufanya hivyo huweka rehani maisha yao kila uchao amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifaifa Antonio Guterres.
Mamilioni waathirika na mabadiliko ya tabianchi Amerika Kusini na Caribbea:WMO
Matukio yanayohusiana na hali ya hewa na jiografia yamesababisha kupoteza maisha ya watu 312,000 na kuathiri moja kwa moja zaidi ya watu milioni 277 katika Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbea kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la hali ya hewa duniani (WMO).
Joto lazidi kuongezeka duniani, binadamu anyooshewa kidole
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema zinahitajika nguvu za pamoja kutoka kwa viongozi wote wa serikali duniani na kwa haraka sana ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayoikabili dunia baada ya ripoti mpya ya wanasayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC iliyotolewa leo kubainisha kuwa shughuli za binadamu zinapeleka dunia katika madhara ya tabianchi yasiyorekebishika.