Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 20 Agosti 2021

Jarida 20 Agosti 2021

Pakua

Hii leo katika jarida utasikia mahojiano na manusura wa Covid-19, Bwana Ole Pertet, mmoja wa wakazi wa Marekani waliougua mwanzoni kabisa ugonjwa huo ulipoingia Marekani. 

Lakini kabla ya mada hiyo utasikia habari kwa ufupi ambapo kuelekea siku ya kimataifa ya kumbukumbu na kuwaenzi waathirika wa ugaidi, itakayoadhimishwa hapo kesho Agost 21, leo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu kuwaenzi waathirika hao ukijikita  zaidi katika msaada wa kisaikolojia na ulinzi kwa waathirika.  

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kwamba mahitaji ya kibinadamu nchini Afghanistan asilani yasisahaulike.  

Na watoto bilioni 1 wameelezwa kuwa katika hatari kubwa ya athari za mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
11'16"