Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

La Ninã inatarajiwa baadaye mwaka huu lakini joto litasalia kuwa juu:WMO

Mabadiliko ya hali ya hewa kwa mfano ukame yanasababisha athari za kiuchumi miongoni mwa wakulima.
UN Photo/Albert Gonzalez Farran
Mabadiliko ya hali ya hewa kwa mfano ukame yanasababisha athari za kiuchumi miongoni mwa wakulima.

La Ninã inatarajiwa baadaye mwaka huu lakini joto litasalia kuwa juu:WMO

Tabianchi na mazingira

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO linatabiri kuongezeka kwa ukame katika baadhi ya maeneo duniani na kuongezeka kwa hatari ya mafuriko katika maeneo mengine.

Jambo hili litasababishja hali ya hewa kuwa mbaya, lakini hata hivyo, joto kati ya mwezi huu wa Septemba na Novemba litakuwa juu ya wastani katika maeneo ya Kaskazini mwa Dunia. 

Hali ya kiwango cha chini cha La Ninã inatarajiwa kuonekana tena mnamo mwaka huu wa 2021, ikiwa ni kwa mwaka wa pili mfululizo.  WMO inatabiri kuongezeka kwa ukame katika sehemu zingine za ulimwengu na kuongezeka kwa hatari ya dhoruba na mafuriko katika maeneo mengine. 

WMO imeyasema hayo katika ripoti yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis kuhusu La Ninã, ambayo ina tabia ya kulainisha joto la uso wa bahari ya Kati na Mashariki mwa Pasifiki.  

Lakini bado, shirika hilo linatabiri kuwa joto kati ya Septemba na Novemba litakuwa juu ya wastani, haswa katika maeneo ya Kaskazini mwa dunia.. 
 

Kaskazini magharibi mwa Somalia wamekuwa wakiathirika na ukame kwa miaka kadhaa sasa
undp Somalia
Kaskazini magharibi mwa Somalia wamekuwa wakiathirika na ukame kwa miaka kadhaa sasa

 Hali ya ukame kutamalaki Afrika 

Shirika lhilo inatabiri mvua zinazohusiana na La Niña, ambayo inapaswa kuwa ya chini kuliko kawaida katika maeneo mengi ya Amerika Kusini na pia katika sehemu nyingi za Mediterania, Rasi ya Arabia na Asia ya Kati. 
Kulingana na WMO, hali ya hewa ya ukame inatarajiwa hadi mwezi Desemba barani Afrika, haswa katika nchi kama Burundi, Kenya, Rwanda na Tanzania. 

Katibu mkuu wa WMO Talasi amesema kuwa "mabadiliko ya tabianchi yanayoathiriwa na vitendo vya wanadamu huongeza athari za majanga ya asili kama La Niña, joto kali na ukame." 

Mwanamke akiembea kwenye maji yaliyotuama katika eneo lililo athirika na mafuriko huko Masharki mwa Jakarta, nchini Indonesia
© UNICEF/Arimacs Wilander
Mwanamke akiembea kwenye maji yaliyotuama katika eneo lililo athirika na mafuriko huko Masharki mwa Jakarta, nchini Indonesia

 

 Amerika Kusini 

Pamoja na kuwasili kwa La Niña, mzunguko wa anga hubadilika, huathiri upepo, shinikizo la hewa na mvua. Kwa ujumla, athari za hali ya hewa ni kinyume cha El Niño, ambayo husababisha joto kali. 

WMO inaonyesha kwamba kuna nafasi ya asilimia 40% ya La Niña kutokea kati ya mwezi Septemba na Novemba na nafasi sawa za kuonekana tena kati ya mwezi Oktoba na Desemba.  

Jambo hilo litachochea hali ya hewa ya joto kati ya Septemba na Novemba mwaka huu , hali ambayo inatarajiwa kuwa juu kuliko kiwango cha wastani Mashariki mwa Amerika Kaskazini, Asia ya kaskazini na Arctic, na pia Mashariki mwa Afrika na kusini mwa Amerika Kusini.   

Sehemu ya mlima Chataltaya nchini Bolivia hapo awali ulikuwa sehemu ya kuchezea barafu lakini katika kipindi cha muongo mmoja limeyeyuka lote ( Maktaba)
World Bank/Stephan Bachenheimer
Sehemu ya mlima Chataltaya nchini Bolivia hapo awali ulikuwa sehemu ya kuchezea barafu lakini katika kipindi cha muongo mmoja limeyeyuka lote ( Maktaba)

 Athari kwa uhakika wa chakula 

Mkuu wa WMO Petteri Taalas pia ameelezea pia kuwa hatari za moto huongezeka, wakati maeneo mengi yanaishia kukumbana na mvua na mafuriko.  

Ameongeza kuwa hii imeonekana katika maeneo kadhaa katika miezi ya hivi karibuni, na "athari zake ni mbaya".  
Taalas amesisitiza kwamba "mabadiliko ya tabianchi yanaongeza kasi ya kiwango cha majanga." 

Mkuu huyo wa WMO amesema kuwa kuboresha mifumo ya tahadhari ya mapema  ya hali ya hewa na usimamizi bora wa maafa ni kuokoa maisha.  

Lakini Taalas amesema athari za kijamii na kiuchumi na kibinadamu zinaongeza ukosefu wa uhakika wa chakula na kusababisha watu zaidi kuyakimbia makazi yao. 

Katibu mkuu huyo wa WMO ameyasema hayo akishiriki mkutano wa ngazi ya juu wa masuala ya kibinadamu kuhusu ushiriki na hatua za masuala yanayotarajiwa  ambao unataka kupanua hatua za pamoja kuhusu mizozo inayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.