Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni waathirika na mabadiliko ya tabianchi Amerika Kusini na Caribbea:WMO

Jamii huko Nicaragua zilitahayari baada ya Kimbunga Iota kuikumba nchi yao Novemba 2020.
© UNICEF/Gema Espinoza Delgado
Jamii huko Nicaragua zilitahayari baada ya Kimbunga Iota kuikumba nchi yao Novemba 2020.

Mamilioni waathirika na mabadiliko ya tabianchi Amerika Kusini na Caribbea:WMO

Tabianchi na mazingira

Matukio yanayohusiana na hali ya hewa na jiografia yamesababisha kupoteza maisha ya watu 312,000 na kuathiri moja kwa moja zaidi ya watu milioni 277 katika Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbea kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la hali ya hewa duniani (WMO). 

Ripoti inasema hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vinatishia eneo lote, la kanda hizo "kutoka urefu wa kilele cha mlima Andes hadi chini kwenye visiwa na mabonde ya mito yenye nguvu.” Imeongeza ripoti hiyo ya “Hali ya hewa Amerika ya Kusini na Caribbea  mwaka 2020". 

Kuongeza kwa kiwango cha joto, mabadiliko ya mifumo ya mvua, dhoruba na barafu zinazoendelea kuyeyuka vyote vimekuwa na athari kubwa kwa afya ya binadamu na usalama, chakula, maji, usalama wa nishati na mazingira. 
"Amerika Kusini na Caribbea (LAC) ni miongoni mwa kanda zenye changamoto kubwa na matukio mabaya ya hali ya hewa," amesema katibu mkuu wa WMO Profesa Petteri Taalas katika taarifa yake kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo. 
 

Sehemu ya mlima Chacaltaya nchini Bolivia hapo awali ulikuwa sehemu ya kuchezea barafu lakini katika kipindi cha muongo mmoja limeyeyuka lote ( Maktaba)
World Bank/Stephan Bachenheimer
Sehemu ya mlima Chacaltaya nchini Bolivia hapo awali ulikuwa sehemu ya kuchezea barafu lakini katika kipindi cha muongo mmoja limeyeyuka lote ( Maktaba)

 
 Madhara makubwa na ya kudumu

Bwana Taalas amebaini athari hizo ni pamoja na "uhaba wa maji na nishati, upotezaji wa kilimo, makazi yao na afya na usalama uliodhoofishwa, na changamoto zote hizi zikizidishwa na janga la COVID-19." 
Wasiwasi juu ya moto na upotezaji wa misitu pia umeibuka katika ripoti hiyo Karibu nusu ya eneo la ukanda wa LAC linafunikwa na misitu, inayowakilisha karibu asilimia 57 ya misitu ya msingi iliyobaki ulimwenguni na kuhifadhi takriban gigatani za hewa ukaa. 
Katibu mkuu wa WMO ameongeza kuwa "Moto na ukataji miti sasa unatishia moja ya ukanda mkubwa ulimwenguni, na athari hizo kubwa ni za kudumu,"  

 
 

Benson Etienne mwenye umri wa miaka 15 na familia yake walikimbia makazi yao kabla nyumba yao haijabomolewa na kimbunga dorian huko eneo la bandari ya March, kisiwa cha Abaco nchini Bahama
© UNICEF/Moreno Gonza
Benson Etienne mwenye umri wa miaka 15 na familia yake walikimbia makazi yao kabla nyumba yao haijabomolewa na kimbunga dorian huko eneo la bandari ya March, kisiwa cha Abaco nchini Bahama

 Ongezeko la joto 

Ripoti hiyo ya WMO imesema mwaka 2020 ilikuwa ni kati ya miaka mitatu yenye joto zaidi Amerika ya Kati na Caribbea na ni mwaka wa pili wenye joto zaidi Amerika Kusini.  
Ongezeko la joto katika kanda zingine limeonyesha kuvunja rekodi na joto kuwa la juu hadi nyuzi joto 10 ° C juu ya kiwango cha kawaida. 

Pia ripoti imeongeza kuwa ukame ulioenea kote Amerika Kusini na Caribbea ulikuwa na athari kubwa, pamoja na kupunguza kiwango cha mito, hali ambayo  imezuia njia za bara za usafirishaji, kupunguza mavuno ya mazao na uzalishaji wa chakula, na kusababisha kuzorota kwa hali ya ukosefu wa chakula katika maeneo mengi. 

Upoteaji wa misitu ni mchangiaji mkubwa kwa mabadiliko ya tabianchi kwa sababu ya kutolewa kwa hewa ukaa, utafiti huo unaonya na kusema kati ya mwaka 2000 na 2016, karibu ekari milioni 55 za misitu zilipotea, ikiwa ni zaidi ya asilimia 91% ya upoteaji wa misitu ulimwenguni. 

Kiwango kilichoongezeka cha moto wa nyika  mnamo mwaka 2020 kilisababisha uharibifu usioweza kurekebishwa kwa mifumo ya ikolojia, pamoja na athari mbaya kwa huduma muhimu za mfumo wa mazingira na maisha yanayotegemewa. Ingawa bado ni kushuka kwa kiwango cha hewa ukaa, eneo la Amazon liko mbioni kuwa chanzo halisiendapo upotezaji wa misitu unaendelea kwa viwango vya sasa. 
 

Kituo cha hali ya hewa cha Marekani mjini Florida, kikionesha taswira ya uharibifu baada ya Kimbunga Dorian huko Bahamas. (2 Septemba 2019)
US Coast Guard Southeast
Kituo cha hali ya hewa cha Marekani mjini Florida, kikionesha taswira ya uharibifu baada ya Kimbunga Dorian huko Bahamas. (2 Septemba 2019)


 Wimbi la joto laendelea kuongezeka 

Mnamo mwaka wa 2020 joto la uso wa bahari ya Caribbea lilifikia kiwango cha juu, na ripoti hiyo inaonyesha jinsi maisha ya baharini, mifumo ya ikolojia ya pwani na jamii za wanadamu zinazotegemea bahari hiyo zinakabiliwa na vitisho vinavyoongezeka kutoka kwa tindikali ya bahari na joto na kuongezeka kwa viwango vya bahari.

Kwa mujibu wa ripoti katika Amerika ya Kusini na Caribbea zaidi ya asilimia 27% ya idadi ya watu wanaishi katika maeneo ya pwani, na inakadiriwa kuwa asilimia 6-8% wanaishi katika maeneo ambayo yako katika hatari kubwa sana ya kuathiriwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi kwenye ukanda wa pwani. 

Barafu zimekuwa zikiyeyuka katika miongo iliyopita, na upoteaji wa barafu umeharakishwa zaidi tangu mwaka 2010, sambamba na kuongezeka kwa msimu wa joto na kila mwaka katika msimu na upunguaji mkubwa wa mvua za kila mwaka katika ukanda huo 
 

Mifumo ya ikolojia ya pwani na baharini hutoa chakula, maisha, na ulinzi wa pwani kwa zaidi ya watu bilioni moja ulimwenguni.
UNCTAD
Mifumo ya ikolojia ya pwani na baharini hutoa chakula, maisha, na ulinzi wa pwani kwa zaidi ya watu bilioni moja ulimwenguni.


 Onyo kwa siku za usoni 

Kujitolea zaidi kisiasa na msaada zaidi wa kifedha inahitajika ili kuimarisha mifumo ya utoaji wa tahadhari ya mapema na utendaji wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, hali ya hewa na huduma za maji, imetanabaisha ripoti hiyo kama njia za kusaidia usimamizi wa hatari na mabadiliko ya tabianchi. 
Mifumo ya tahadhari ya mapema inaweza kupunguza athari za maafa na athari zingine lakini utafiti wa WMO unaonya kuwa mifumo hiyo haijaendelea katika ukanda wa LAC, haswa Amerika ya Kati na Kusini. 
Mikoko huchaguliwa kama rasilimali ya kipekee ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na uwezo wa kuhifadhi hewa ukaa mara tatu hadi nne kuliko misitu mingi duniani. 
Walakini, eneo la mikoko katika ukanda huo lilipungua kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2001-2018. Uhifadhi na urejeshwaji wa mifumo iliyopo ya "khewa ukaa ya samawati" kama vile mikoko, matumbawe na mabwawa ya chumvi hutambuliwa kama fursa muhimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto duniani. 

 

 Kuhusu utolewaji wa ripoti hiyo 

Ripoti hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa WMO, ECLAC, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji wa majanga UNDRR
Ripoti hiyo inalenga kutoa taarifa za kisayansi kuzisaidia nchi na jamii katika juhudi za kujenga mnepo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi na matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotarajiwa.