Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Imetosha kupiga domo ni wakati wa kuonyesha vitendo kukabili mabadiliko ya tabianchi:UN
Macho na masikio ya dunia sasa yako Glasgow, Scotland, wakati mkutano wa viongozi wa dunia ukifunguliwa na leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26.
1 Novemba 2021
Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tunaelekea Glasgow Scotland ambako kunafanyika mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi au COP26.
COP26 ikifungua pazia WMO yasema miaka 7 iliyopita imevunja rekodi ya joto duniani
Miaka saba iliyopita inaelekea kuwa ya joto zaidi kuwahi kurekodiwa sanjari na kupanda kwa kina cha bahari ni katika viwango vya kuvunja rekodi, kulingana na ripoti ya muda ya shirika la hali ya hewa duniani (WMO) ya hali ya hewa duniani kwa mwaka 2021, iliyotolewa Jleo umapili, wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26, ukifunguliwa Glasgow, Uingereza.
Tukiadhimisha siku ya miji tudhibiti hatari za mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo:UN
Leo ni siku ya miji duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mastaifa amesema ingawa kupanda kwa kina cha bahari kunaweza kuweka zaidi ya watu milioni 800 katika miji ya pwani kwenye hatari ya moja kwa moja ifikapo mwaka 2050, chini ya asilimia 10 ya fedha za mabadiliko ya tabianchi kwa maeneo ya mijini zinakwenda katika hatua za kukabiliana na kujenga mnepo.
COP26 – Tunachofahamu kwa sasa, na kwa nini ni muhimu: Muongozo wako wa habari kutoka Umoja wa Mataifa
Katika dunia iliyotikiswa na mliipuko na kuwa dirisha lililofuga fursa za kupambana na majanga ya tabianchi, mkutano muhimu wa Umoja wa Mataifa wa COP26 unang’oa nanga leo Jumapili katika mji wa Glasgow nchini Scotland madhara ya janga hilo yasingekuwa makubwa zaidi kama yalivyo sasa.
Wakuu wa G-20 onyesheni uongozi kuokoa maisha:Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehudhuria ufunzi rasmi wa mkutano wa viongozi wa mataifa 20 yaliyoendelea kiuchumi duniani G-20 .
Ukweli ulio wazi ni kwamba dunia inaelekea kwenye zahma ya mabadiliko ya tabianchi:Guterres
Tuko katika wakati muhimu kwa sayari yetu. Lakini wacha tuwe wazi kuna hatari kubwa ambayo mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa Glasgow unaweza usizai matunda, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo akizungumza na waandishi wa Habari mjini Roma Italia kunakofanyika mkutano wa mataifa 20 yaliyoendelea kiuchumi duniani au G-20.
Ni wakati wa kuchukua hatua haraka kwa ajili ya maji na mabadiliko ya tabianchi
Mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO na mashirika mengine tisa ya kimataifa yametoa wito wa pamoja na wa dharura kwa serikali kuweka kipaumbele kwa hatua jumuishi za maji na mabadiliko ya tabianchi kutokana na athari zinazoenea za masuala hayo kwa maendeleo endelevu.
29 Oktoba 2021
Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ijumaa tunakuletea mada kwa kina leo tukimulika usanifu majengo na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi mijini kuelekea siku ya miji duniani tarehe 31 mwezi huu wa Oktoba.
Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia wito uliotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani na mashirika mengine ya kimataifa tisa kuhusu maji na mabadiliko ya tabianchi. Taarrifa nyingine ni Maendeleo ya teknolojia kwa wanahabari na asasi za kiraia pamoja na mbinu bora na za kimkakati za kuwalinda watoto walioathiriwa na migogoro
Jipime ufahamu wako kuhusu COP26
Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 unafanyika Glasgow, Scotland. Je unafahamu kwa kiwango gani yanayojadili? Hapa kuna fursa ya kujaribu uelewa wako kupitia maswali yetu kwako kuhusu mabadiliko ya tabianchi. (Majibu yako chini kabisa ya ukurasa huu)