Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

14 Januari 2021

Hii leo jaridani kwa kiasi kikubwa ni masuala ya mabadiliko ya tabianchi tukimulika ripoti ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, kuhusu hatua thabiti za kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kutumia mbinu za asili, halikadhalika ripoti kuhusu viwango vya joto kutoka shirika la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa, WMO, ikiutaja mwaka 2020 kuwa moja ya miaka mitatu iliyoongoza kwa kuwa na viwango vya juu sana vya joto duniani. Tunakwenda pia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambako mapigano mapya yamesababisha vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua.

Sauti
10'53"

05 JANUARI 2021

Katika Jarida la Habari za UN hii leo Flora Nducha anakuletea

-Wakimbizi kutoka Tigray Ethiopia waendelea kumiminika Sudan na mahitaji yao yanaongezeka lasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR

-Kutana na Muhamiaji Mohammed Bushara ameye alienda Libya kusaka mustakbali bora lakini sasa amerejea nyumbani kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na Muungano wa Ulaya Eu na kuanzisha biashara ya duka la vipodozi

Sauti
11'32"

21 DESEMBA 2020

Hii leo jaridani ni mada kwa kina na tunakwenda mkoani Mwanza nchini Tanzania ambako shirika la Amani girls home wameanzisha mradi unaowawezesha wasichana hususani wale waliokumbwa na changamoto mbalimbali za kimaisha, ili waweze kufikia malengo yao kwa kuwapa ujuzi mbalimbali. Lakini tuna Habari kwa Ufupi ikimulika Burkina Faso, Mali na kubabuka kwa matumbawe Mashinani tunabisha hodi DRC. Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda.

Sauti
11'25"
FAO/Rudolf Hahn

Mabadiliko ya tabianchi, tishio kwa eneo la bonde la ufa Kenya

Kuongezeka kwa maji kwenye maziwa yaliyo eneo la bonde la ufa nchini Kenya ni jambo ambalo linaendelea kuzua wasiwasi miongoni mwa watu wa maeneo hayo na pia pigo kubwa kwa sekta muhimu ya utalii nchini Kenya. Serikali imekuwa ikiwashauri wale wanaoishi karibu na maeneo hayo kuhama na kujitafutia sehemu salama huku ikitafuta suluhusu ikiwa maji hayo yatazidi kuongezeka siku zinazokuja. Mwandishi wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na mtaalamu wa hali ya hewa nchini Kenya Henry Ndede kutaka kufahamu chanzo ni kipi.

Sauti
2'38"
Mkutano wa 26 wa kimataifa wa mbadiliko ya tabianchi COP26 uliokuwa ufanyike baadaye mwaka huu umehairishwa.
Unsplash/Adam Marikar

Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi umeishaje, na nini kinafuata?

Wakuu wa nchi na serikali zaidi ya 70 , wakiwemo pia viongozi wa kikanda, mameya wa miji mbalimbali na wakuu wa mashirika mbalimbali duniani wamewasilisha hatua wanazotarajia kuchukua ili kupunguza kiwango cha hewa chafuzi ya viwandani na kuzuia dunia kuendelea kuchemka na ongezeko la joto katika mkutano wa matamanio ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi uliomalizika Jumamosi jioni.