Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Tukihifadhi mazingira leo tunaepuka gharama kubwa Kesho

Wana mradi wa kuruwitu kutoka Kilifi Mombasa nchini Kenya, wametoa wito wa kuhifadhi mazingira leo ili kuepuka athari zake katika kizazi kijacho. Shida Magunda na Katana Ngala Hinzano wako katika mradi wa kuhifadhi mazingira ya bahari Mombasa kwa kutumia uzalishaji wa samaki. Mradi wao ambao ni wa kwanza nchini Kenya pi umetunukiwa tuzo ya mazingira ya Equator inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Equator initiative. Wamezungumza na Flora Nducha na Katana Ngala anaanza kueleza historia ya mradi

Nilikuwa muathirika wa FGM lakini sasa mimi ni mshindi- Inna Modja

Ukatili wa aina yeyote dhidi ya wanawake na wasichana hauna nafasi katika dunia hivi sasa kwani unakwamisha mendeleo. Yaelezwa kuwa ili kukabiliana na ukatili huo ni lazima kufahamu sura ambazo unachukua ili kuweza kukabiliana nao.

Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii ambapo mwanamuziki Inna Modja kutoka Mali anatuma ujumbe kutumia muziki akisema kwamba yeye binafsi aliwahi kuwa muathirkia wa ukatili dhidi ya wanawake.

Hedhi salama ni muarobaini katika kumuokoa msichana- Rebecca

Vijana ndio tegemeo kubwa hivi sasa la Umoja wa Mataifa katika kusaka suluhu za changamoto zinazokumbwa ulimwengu. Ni kwa kutambua hilo chombo hicho chenye nchi wanachama 193 kinatumia uthabiti wa kundi hilo kuleta mabadiliko mashinani kwa kutambua uwezo wa vijana katika kuelewa na kuabdili maisha yao na ya wenzao. Kwa mantiki hiyo kando ya mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, viongozi vijana kutoka nchi mbali mbali walipata fursa ya kukutanishwa na viongozi walio madarakani hivi sasa ili kujadili mustakhbali wa dunia.

Ukame waathiri usafiri wa majini kupitia Ziwa Albert Uganda

Mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika masuala mbalimbali ikiwemo huko nchini Uganda ambako mwaka huu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa nchi ambazo zimekabiliwa na ukame wa muda mrefu.

Kando na kusababisha njaa katika nchi za Afrika Mashariki pia moja ya athari ni kupungua kwa kiwango cha maji katika Ziwa Albert tangu Machi kulikokwamisha usafiri wa majini.Basi ungana na John Kibego katika makala hii inayokupa taswira ya hali ilivyo kwa sasa.

Haikuwa rahisi,wakimbizi wa Burundi waanza kurejea nyumbani: UNHCR

Hatimaye kundi la kwanza la wakimbizi wa Burundi walioko nchini Tanzania limewasili nchini mwao, hii ni baada ya sintofahamu iliyosababisha mkutano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, serikali ya Tanzania na Burundi.

Urejeshwaji wa wakimbizi hao kwa hiari umeanza kutekelezwa ambapo wakimbizi 300 wamewasili Burundi kurejelea maisha kwa kile kinachoaminika kuwa ni usalama kuimarika nchini mwao.

Picha: UM/Video capture

Watu wa Asili kushirikishwa katika utekeleshwaji wa SDGs: Laitaika Sehemu ya 2

Mwaka huu ni miaka kumi tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kwenye Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Tangu wakati huo kuna hatua kubwa zimepigwa hususani barani Afrika has kuwatambua watu wa asili lakini pia kufahamu kuhusu azimio hilo la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji wa baadhi ya haki hizo zinazojumuisha , afya, elimu, ajira , sheria na nyinginezo.

Kuna hatua, lakini safari ni ndefu kutimiza haki za watu wa asili: Laitaika Sehemu ya 1

Mwaka huu ni miaka kumi tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kwenye Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Tangu wakati huo kuna hatua kubwa zimepigwa hususani barani Afrika has kuwatambua watu wa asili lakini pia kufahamu kuhusu azimio hilo la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji wa baadhi ya haki hizo zinazojumuisha , afya, elimu, ajira , sheria na nyinginezo.

Fursa na vikwazo katika juhudi za vijana kujikwamua nchini DRC 1

Katika mfululizo wa makala zinazomulika juhudi za vijana katika kujikwamua kiuchumi, tunakupeleka Afrika Mashariki kusikiliza mahojiano na  kijana mjasiriamali Kiiza Serugendo Elwa kutoka mji wa Kiwanja, Jimboni Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Ungana na John Kibego katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano na kijana huyu ambaye kwa sasa yuko nchini Uganda.

(MAHOJIANO)

Kaa chonjo kusikiliza sehemu ya pili ya makala haya juma lijalo.